Jumatano 24 Septemba 2025 - 08:39
Ulaya yaungana kwa ajili ya kuiunga mkono Ghaza

Hawza/ Mashindano, tamasha na mikusanyiko mbalimbali barani Ulaya vinaonesha ongezeko la chuki ya umma dhidi ya Israel muhalifu, Mabango na bendera zinazoashiria upinzani kwa wachezaji wa timu za Israeli vimekuwa vikibebwa mikononi mwa watu katika viwanja vya michezo.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya  Shirika la Habari la Hawza, kuanzia mashindano ya baiskeli nchini Uhispania hadi mashindano ya mpira wa vikapu nchini Poland, katika matukio mengi ya michezo, wananchi wamekuwa wakionyesha ghadhabu zao na chuki dhidi ya Israel, harakati za kuipinga na kuisusia Israel zinaongezeka kila siku.

Mashindano ya baiskeli nchini Uhispania yalivurugwa na wananchi kutokana na uwepo wa washiriki wa Israeli, huku nchini Poland watu walikata wimbo wa taifa wa Israel kabla ya pambano la mpira wa vikapu, wakionya kuwa endapo utachezwa tena, wataukata pia wimbo wa taifa wa timu za Ulaya.

Matukio haya yanaashiria hali ya kutengwa kwa kiwango ambacho Israel haijawahi kukipata duniani, idadi kubwa ya washiriki na watazamaji wametoa wito wa kufungiwa timu za Israeli kushiriki kwenye mashindano, sawa na jinsi timu za Urusi zilivyofungiwa mwaka 2022.

Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sánchez, pia alionyesha kuunga mkono wananchi waliovuruga mashindano ya baiskeli kupinga ushiriki wa Israel, jambo lililowafanya Waisraeli kuingia kwenye wakati mgumu zaidi.

Hata hivyo, FIFA bado inachelewesha kujadili suala la kuifungia na kuisusia Israel, baadhi ya wachezaji wa Ulaya wanaocheza katika timu za Israeli wamedai kwamba FIFA inawalazimisha kuendelea kucheza kwenye timu hizo ili kuzuia kususia kwa kiwango kikubwa.

Licha ya hali hii, wananchi kutoka tabaka mbalimbali wanataka kuisusia Israel, hata baadhi ya wasanii wa Hollywood wameahidi kuzisusia taasisi za filamu za Israeli.

Chanzo: Al-Mayadeen

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha