Kwa mujibu wa ripoti ya kitengi cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Taqiy Mudarrisi, mmoja wa wanazuoni wa Iraq, ataka vyombo vya habari vinavyo ongopa vipigwe marufuku, na akavieleza kama "nguvu kuu" inayodhibiti fikra za umma na kwa ujanja, inawalazimisha wanyonge kwa uongo wao ili kuwafanya watumwa.
Ayatullah Mudarrisi katika hotuba yake ya kila wiki ya kimaadili aliyotoa kwa wanafunzi wa Hawza Karbala al-Mu‘alla, alisisitiza kuwa vyombo vya habari vimekuwa nguvu kuu ya kudhibiti fikra za watu kote duniani, na uongo wao wa kupotosha wanauwalazimisha mataifa wanyonge kwa hoja za kijanja na za udanganyifu ili kuwafanya watumwa.
Alisema kuwa: Vyombo vya habari vya vibaraka vinajitahidi katika nchi zetu kuficha uovu wa nchi za kidhalimu ambazo zimeiba rasilimali za watu na kudhibiti nyanja zote za maisha yao ya kibinafsi, kisiasa na kiuchumi. Kinyume chake, vinaibua matatizo ya nchi zilizoko chini ya ukoloni ili kugeuza fikra za watu dhaifu kuelekea matatizo yanayotokana na uvamizi na dhulma za wavamizi, hata hivyo, sababu za kweli na za kimsingi zinazotokana na njama ovu za maadui hupuuzwa.
Ayatullah Mudarrisi alitaka kuingia kwenye uwanja wa changamoto za kimedani na kukabiliana na uongo, na alisisitiza kuwa vyombo vya habari vya Kishia katika historia vimewapa changamoto mataghuti na kuwa na athari kubwa zaidi kuliko vyombo vya habari vya kitaghuti na vya vibaraka.
Mwanazuoni huyu wa Iraq alibainisha: Tunapaswa kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, kusimama imara na kukataa uongo wa vyombo vya habari, kupambana na vyombo vya habari vya kidhalimu, tunapaswa kupata taarifa zetu kutokana na ukweli tunaoushuhudia na sisi wenyewe kuuona, na siyo kutoka kwa vyombo vya habari vya vibaraka.
Maoni yako