Kwa mujibu wa taarifa ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangaza rasmi kwamba imetoka katika mfumo wa awali wa vikwazo (SDGT) vinavyohusu masuala ya kifedha na kiuchumi na kuipandisha katika daraja la FTO ambalo linahusisha adhabu na matokeo ya kiusalama na jinai.
Kwa mujibu wa marekebisho haya, serikali ya Marekani imeitambua rasmi Nujabaa kama taasisi ya kigeni ambayo katika uga wa usalama na maslahi ya taifa, inachukuliwa kuwa tishio halisi kwa Marekani na washirika wake kama vile Israel.
Miongoni mwa vipengele vya mfumo huu mpya wa vikwazo, ni kuhalalishwa kwa uhalifu na kufunguliwa mashtaka ya jinai dhidi ya watu au mashirika yoyote yatakayotoa msaada kwa Nujabaa au baadhi ya makundi mengine ya muqawama ya Iraq.
Mfumo huu wa vikwazo unatajwa kuwa ndio chombo kikali zaidi cha kidiplomasia cha Marekani katika kukabiliana na mashirika ambayo inayaona kama “tishio kubwa kwa usalama wa dunia.”
Kwa hakika, hatua hii ya Washington ni ujumbe kwa Nujabaa kwamba kuanzia sasa itachukuliwa kama shirika huru (sio tena kundi la kupokea maagizo ya kiwakala) linalotishia usalama wa taifa la Marekani, na wanachama wake, wafuasi na washirika wake hawatakuwa salama na watakabiliwa na adhabu kwa kosa la kushirikiana na muqawama.

Maoni yako