Jumapili 24 Agosti 2025 - 00:18
Mwanazuoni mashuhuri wa Kashmiri: Shahada ni kilele cha ubinadamu na ngome imara mbele ya dhulma na ufisadi

Hawza/ Hujjatul-Islam Sayyid Hadi Musawi, katika maelezo yake kuhusu falsafa ya shahada, alifafanua daraja tukufu la shahidi na kusisitiza umuhimu wa kujitolea, kusimama imara dhidi ya dhulma na kudumu maisha ya kiroho ya mashahidi

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hadi Musawi, mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Kashmir, katika kikao kikubwa cha maombolezo, alifafanua falsafa ya shahada na kuzungumzia nafasi ya juu ya shahidi katika mfumo wa Uislamu, huku akisisitiza umuhimu wa kujitolea, kusimama imara dhidi ya dhulma na kudumu maisha ya kiroho ya mashahidi.

Katika hotuba zake, huku akibainisha kwamba “Shahada kwa hakika ni miraji ya mwanadamu na kilele cha uja wa Mola”, alisema: Shahidi ni mtu anayesimama kwa ajili ya haki, anatengeneza maisha kwa ajili ya dini na mwishowe hutoa nafsi yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, Qur’ani Tukufu pia imeeleza wazi: “Wala msiwadhanie kuwa wafu wale wanaouliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu; bali wao wako hai, wanaruzukiwa kwa Mola wao”.

Mwanazuoni huyu wa Kashmiri, akiashiria hamasa ya daima ya Ashura, alisisitiza: Karbala imetufundisha kuwa damu ya shahidi ni yenye nguvu zaidi kuliko upanga, Imam Husein (a.s) na wafuasi wake waaminifu walionyesha kwamba; kusimama dhidi ya dhulma ni heshima na kunyenyekea mbele ya batili ni fedheha, shahidi kwa kumwaga damu yake, huupa tena uhai umma na kuiita jamii kuelekea kwenye uhuru na mapambano.

Hujjatul-Islam Sayyid Hadi Musawi pia, akisisitiza ujumbe wa milele wa kujitolea kwa mashahidi, alibainisha: Sadaka ya shahidi inaonyesha kwamba raha na mandhari ya kidunia ni vya kupita na vya muda mfupi, lakini imani, ukweli na kujitolea ni vya kudumu na vya milele, damu ya shahidi katika kila zama imekuwa ngome imara mbele ya fitna na ufisadi na daima imeinusuru jamii ya kibinadamu kutokana na kuporomoka na kuangamia.

Mwisho, akiwahutubia washiriki, alisema: Wajibu wetu ni kuufanya mwenendo wa mashahidi kuwa kigezo cha maisha yetu, shahidi hata baada ya kufa bado yu hai na huiongoza jamii ya Kiislamu kuelekea maisha ya kweli na heshima ya milele, ikiwa tunataka kuwa na jamii yenye mwamko, yenye mapambano na yenye heshima, ni lazima tuifanye njia ya mashahidi kuwa kielelezo cha maisha yetu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha