Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, siku chache zilizopita watumiaji waligundua kuwa akili mnemba "Grok" ilipoulizwa kuhusu iwapo mauaji ya kimbari yametokea Ghaza, ilisema: “Ndiyo, Israel na Marekani wanafanya mauaji ya kimbari huko,” na ilipoulizwa sababu ya kauli hiyo, ilikuwa ikinukuu ripoti za Umoja wa Mataifa, UNICEF, UNESCO na B’Tselem kuhusu uhalifu wa Israel huko Ghaza.
Akili mnemba "xAI Grok" ni miongoni mwa bidhaa za kampuni ya Elon Musk, Hata hivyo baada ya muda mfumo huo ukasitishwa, na uliporejeshwa tena, katika jibu kuhusu mauaji ya kimbari ya Israel ulisema kuwa hakuna ushahidi wa mauaji ya kimbari yaliyothibitishwa!
Chanzo: TRT GLOBAL
Maoni yako