Jumanne 12 Agosti 2025 - 10:07
Sehemu ya kuabudia Waislamu yenye umri wa miaka 600 yagunduliwa chini ya ardhi

Hawzah/ Sehemu ya kuabudia Waislamu ya kale yenye umri wa takribani miaka 600 imegunduliwa katika moja ya maghala ya chini ya ardhi ya kuhifadhia mbao nchini Uturuki.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, ugunduzi huu umefanyika katika kijiji cha Taşkinpaşa kilichoko katika eneo la mkoa wa Niğde, Uturuki, kadirio la utangu wa jengo hili na utambuzi wake vimefanywa na baadhi ya wanahistoria kutoka Chuo Kikuu cha Sanaa na Sayansi cha mji wa Niğde.

Kulingana na alama za usanifu zilizopo katika jengo, inaweza kusemwa kuwa linahusiana na kipindi cha karne ya kumi na sita.

Wataalamu wa akiolojia, baada ya msimamizi wa jengo hilo kuwapa ruhusa ya kulichunguza na kuingia katika eneo hilo, walibaini kuwa kwa muda mrefu jengo hili la kihistoria, kutokana na kutojua umuhimu wake, limekuwa likitumika kama ghala la mbao. Jengo hili liko chini ya ardhi.

Wataalamu hao, baada ya kulisafisha kitaalamu na kuliondoa uchafu kwa kutumia vifaa maalumu, waligundua kuwepo kwa kitabu chenye michoro ya mapambo kilichochongwa, ambacho kwa alama maalumu kinaonyesha upande wa Makka.

Profesa Savaş Maraşlı, mmoja wa wajumbe wa timu ya utafiti, alisema: “Hili ni jengo la kihistoria lenye umri wa miaka 600, na kufichwa kwake kumepelekea liwe salama na kuhifadhiwa vizuri. Siri za usanifu wake zinaonyesha kuwa linahusiana na kipindi cha Waselejuk.”

Chanzo: Turkey Today

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha