Jumapili 10 Agosti 2025 - 16:22
Maandamano makubwa na yenye haiba ya kipekee, yafanyika kwa ajili ya kuiunga mkono Ghaza na kulaani jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni huko Kargil

Hawza/ Kufuatia kuendelea kwa jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni, kufukuzwa kwa lazima na kuzingirwa watu wa Ghaza, Taasisi ya Kumbukumbu ya Imam Khomeini (r.a) huko Kargil, India, iliandaa maandamano makubwa na kutangaza kuliunga mkono taifa la Palestina lenye kudhulumiwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kufuatia kuendelea jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni, kufukuzwa kwa lazima na kuzingirwa watu wasio na ulinzi wa Ghaza, Taasisi ya Kumbukumbu ya Imam Khomeini (r.a) katika mji wa Kargil, India, iliandaa maandamano mapana na yenye haiba kubwa yakiwa na lengo la kutangaza kuliunga mkono taifa la Palestina lenye kudhulumiwa.

Maandamano haya, ambayo yalianza yakiwa na kaulimbiu isemayo: “Kusimama kidete dhidi ya maadui wa Uislamu; Marekani, Israel na Uingereza”, yalihudhuriwa na maelfu ya watu kutoka tabaka mbalimbali za wananchi, msafara wa waandamanaji ulianza katika uwanja wa "Zainabiya" na baada ya kupitia njia iliyopangwa, ulimalizika mbele ya "Msikiti Mkuu wa Kargil".

Washiriki walikuwa wamebeba mabango yenye kaulimbiu za kuiunga mkono Palestina na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni, na kwa sauti za kupinga mauaji ya halaiki na uvamizi wa Israel, walionyesha mshikamano wao na mapambano ya Palestina, mazingira ya mkusanyiko huo yalijaa hisia za kidini, kibinadamu na misimamo ya kupinga ubeberu.

Miongoni mwa mambo yaliyovutia katika maandamano hayo ni ushiriki mkubwa wa wanafunzi wa shule zilizo chini ya usimamizi wa "Jumuiya ya Elimu ya Murtahari". Vijana hawa, wakiwa wamebeba mabango na wakipaza sauti za kuunga mkono dhana ya uhuru wa Palestina, walidhihirisha mshikamano wa kizazi kipya na taifa la Palestina lenye kudhulumiwa.

Mkusanyiko huu mkubwa, mbali na kuonesha uhusiano wa kina wa watu wa Kargil na taifa la Palestina, ulipeleka ujumbe ulio wazi na wa nguvu kwa madola ya kibeberu na wale wanaounga mkono utawala wa Kizayuni kwamba, mataifa huru duniani hayatanyamaza kamwe mbele ya dhulma, uvamizi na jinai, na daima yatasimama pamoja na haki na uadilifu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha