Jumatatu 4 Agosti 2025 - 04:40
Kwa nini tunaghafilika sisi wenyewe?

Hawza/ Allamah Hasan Zadeh (ra) ameeleza kuwa kuitambua nafsi ndilo suala muhimu zaidi la maarifa, kwa sababu maarifa ya Mwenyezi Mungu yanategemea na kujitambua, alionya kwamba kupuuza ukubwa wa uwepo wa mwanadamu kunamfanya binadamu kuwa kama mnyama anayeshughulika tu na maisha ya kimaada.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Allamah Hasan Zadeh (ra) alisisitiza kwamba maarifa ya nafsi ndilo jambo la msingi zaidi, kwani maarifa ya mwanadamu kwa Mola wake yanajengwa juu ya kuitambua nafsi.

Amesema kuwa: “Kitu cha pekee kinachotufaa zaidi kuliko vyote ni sisi wenyewe tujitambue.”

Aliongeza kuwa mtu ambae haijali nafsi yake ni kama vile ameacha mche wa uwepo wake ukuwe ovyo kama nyasi bila mpangilio, inaonyesha kuwa hajui yeye ni kiumbe mwenye ukubwa kiasi gani.

Allamah Hasan Zadeh aliendelea kufafanua kuwa mwanadamu hapaswi kuwa mjinga kuhusu nafsi na hali zake, na kuishi katika ulimwengu wa wanyama, akijisahau mwenyewe, kama sisimizi ambaye mawazo na juhudi zake zote zipo katika kutafuta maisha ya kimaada pekee.

Chanzo: Ishara Mia na Kumi za Allamah Hasan Zadeh

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha