Jumamosi 2 Agosti 2025 - 09:49
Mwanasiasa wa Kanada: Propaganda za Israel dhidi ya Hamas zimeimarisha chuki dhidi ya Uislamu nchini Kanada

Hawza/ Bi. Amira Alghawabi, mwakilishi maalumu wa Kanada kwa ajili ya kupambana na chuki dhidi ya Uislamu katika nchi hiyo, ameonya kwamba; kwa masikitiko propaganda za jinai za Israel dhidi ya Hamas na vita vya Ghaza zimesababisha kuimarika kwa mitazamo ya chuki dhidi ya Uislamu katika nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Bi. Amira Alghawabi ambaye anatoka katika jimbo la Ottawa nchini Kanada, ameonya kwamba hali ya hivi karibuni na propaganda za Israel dhidi ya Uislamu na Hamas nchini Kanada zimesababisha mawazo potofu na mitazamo yenye chuki, ambayo ilienea wakati wa tukio la Septemba 11, ambapo Waislamu walionekana kama magaidi, kujitokeza upya kwa nguvu nchini Kanada.

Kwa masikitiko, tunaona kwamba waandishi wa kurasa za magazeti na vyombo vya habari wanataja maandamano yoyote ya kuunga mkono watu wanyonge wa Ghaza kama maandamano ya chuki, na hili lina maana kwamba mkono wa utawala wa Kizayuni katika operesheni ya vyombo vya habari unaonekana waziwazi.

Hilo lipo hivyo, hali ya kuwa nikizungumza na maafisa wa polisi, wao wanasema: “Sisi tunaona kwamba maandamano mengi ya kuunga mkono Ghaza ni ya amani na yanafanyika bila hotuba zinazohamasisha vurugu.”

Ameongeza pia: “Hali ya dharura ya Ghaza na kuzingirwa kwake ni ya kutia wasiwasi sana; watu wa Ghaza wamenyimwa hadi maji na chakula!”

Bado Wakanada wengi wanaamini kwamba huko Ghaza na Palestina, dhulma na jinai za kutisha zinatokea kutoka kwa Israel.

Chanzo: CTV NEWS

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha