Jumatatu 28 Julai 2025 - 07:05
Allama Hasan Zadeh Amoli: Maisha ya milele yapo mbele yetu; Usijisahau mwenyewe

Hawza/ Ewe kiumbe bora, usijisahaulishe; uwepo huu wa thamani kubwa ni kazi ya kipekee ya Mwenyezi Mungu, ukimsahau Mungu, utajisahau mwenyewe pia, na huo ndio mwanzo wa kuanguka, basi jihadhari, kila kitu kabla ya kukikubali kichunguze: maneno, rafiki, meza ya chakula, sahihi, nyumba hii ina mwenyewe.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, marehemu Allama Hasan Zadeh Amoli katika moja ya hotuba zake alisisitiza juu ya mada ya “kujisahau, kumsahau Mungu” ambayo inawasilishwa kwenu kama ifuatavyo:

Ewe Kiumbe Mkubwa Zaidi wa Mwenyezi Mungu, Jitambue

Ndugu yangu, dada yangu, mwanangu, binti yangu, vipenzi vyangu, taji la kichwa changu:

Tazama uso wako, asili yako, muundo wa uwepo wako, na vyote vinavyojiri katika uwepo wako; vyote hivi ni kazi ya Mwenyezi Mungu.

Usijisahau.

«وَلا تَکُونُوا کَالَّذِینَ نَسُوا اللَّهَ فَأَنسَاهُمْ أَنفُسَهُمْ ۚ أُولَٰئِکَ هُمُ الْفَاسِقُونَ»

Msiwe kama wale waliomsahau Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu akawafanya wajisahau wao wenyewe, hao ndio mafasiki.

(Suurat H'ashir aya 19)

Msijisahau wenyewe.

Uwepo huu, ni kiumbe kikubwa zaidi cha Mwenyezi Mungu.

Ewe kiumbe bora wa Mwenyezi Mungu, Usijichafue, jihadhari.

Ichunge nafsi yako.

Yanuse maneno
Kinuse chakula
Inuse sahihi
Mnuse rafiki
Inuse meza ya chakula

Je, umemuona mbwa na paka?

Kabla ya kula chakula, wanakinusa, muda wa kuwa hawaja kinusa, muda wa kuwa hawaja kihakikisha, hawawezi kufungua mdomo, hawali chakula.

Nyumba ina mwenyewe, maisha ya milele yapo mbele yetu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha