Jumatatu 28 Julai 2025 - 06:55
Sheikh Mkuu wa TIC: Tumuenzi sheikh Hassan Mwalupa na Sheikh Abdillah Nasir kwa kusomesha na kuhuisha kazi zao walizozifanya

Hawza/ Sheikh Hemed Jalala amesisitiza kuwa; Tukitaka kumuenzi sheikh Hassan Mwalupa na Sheikh Abdillah Nasir ni wajibu wetu kusomesha na kuhuisha kazi zao walizozifanya masheikh hawa

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, amesisitiza kuwa njia bora ya kuwaenzi masheikh mashuhuri wa Kiislamu kama vile, Sheikh Hassan Ali Mwalupa na Sheikh Abdillah Nasir, ni kwa kuendeleza elimu walizo zitoa kipindi cha uhai wao, kufundisha na kuhuisha kazi zao walizozifanya kwa umma wa Kiislamu, maulana Sheikh Hemed Jalala, aliyasema hayo katika Khitma (Hauli) ya kumkumbuka Mar’houm Samahat Sheikh Hassan Ali Mwalupa, iliyofanyika Matuga katika Kaunti ya Kwale nchini Kenya.

Sheikh Mkuu wa TIC: Tukitaka kumuenzi sheikh Hassan Mwalupa na Sheikh Abdillah Nasir ni wajibu wetu kusomesha na kuhuisha kazi zao walizozifanya masheikh hawa.

Baadhi ya Msheikh na waumini mbali mbali walio hudhuria katika hafla hiyo

Katika hotuba yake, alieleza kuwa mchango wa masheikh hao wawili katika kueneza elimu ya dini na kufafanua mafundisho ya Kiislamu ni urithi adhimu unaopaswa kuendelezwa na vizazi vijavyo. Aliongeza kuwa, juhudi za kuendeleza kazi zao ni jukumu la kila Mwislamu anayetambua nafasi ya wanazuoni hao katika historia ya Uislamu nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Sheikh Hemedi Jalala katika kuhitimisha hutuba yake, aliwataka waumini na taasisi za Kiislamu kuhakikisha kuwa maandiko, mihadhara, na mafundisho ya masheikh hao yanahifadhiwa, kufundishwa na kuenezwa katika vizazi vijavyo ili kuendelea kuwanufaisha Waislamu wote.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha