Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kufuatia ongezeko la takwimu za uhalifu unaochochewa na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu nchini Uingereza, serikali ya nchi hiyo imeiagiza taasisi ya BMT kufuatilia mafaili hayo hadi pale bajeti ya taasisi ya "Tell MAMA", ambayo ilikuwa taasisi kuu ya kushughulikia uhalifu huo, itakapopatikana tena.
Taasisi ya BMT iko chini ya uongozi wa "Akeela Ahmed", na inatarajiwa kuanza rasmi kazi zake kwa uzito mkubwa kuanzia mwanzoni mwa msimu wa vuli wa mwaka huu.
Bwana Ahmed katika hotuba yake alisema: “Kwa masikitiko, kutokana na kukosekana kwa imani ya wananchi, tumeona kwamba kwa muda sasa uhalifu na malalamiko hayaripotiwi, lakini sasa hakuna haja tena ya kuwa na wasiwasi, Taasisi yetu ni mpya kabisa yenye nguvu mpya na iko tayari kushughulikia matatizo, uhalifu na malalamiko yanayotokana na chuki dhidi ya Uislamu.”
Akaongeza kuwa: “Tumeandaa mfumo mpya ambao unaruhusu kusajili malalamiko, iwe kwa njia ya mtandaoni au nje ya mtandao, ninasisitiza kuwa jukumu letu ni kusikiliza sauti ya watu na kuiwasilisha sauti hiyo mbele ya jamii!”
Kuanzishwa kwa taasisi ya BMT kumeunda msingi muhimu katika kuimarisha hisia za usalama na kushughulikia malalamiko ya jamii ya Kiislamu nchini Uingereza.
Chanzo: The Guardian
Maoni yako