Ijumaa 18 Julai 2025 - 08:34
Kimya kinacho oneshwa na taasisi za kimataifa mbele ya vitendo vya Israel hakikubaliki

Hawza/ Muhammad Sarwat Ijaz Qadiri, katika hotuba yake, ameikosoa vikali Jumuiya ya Kimataifa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kwa kukaa kimya mbele ya jinai zinazofanywa na Israel, na ametoa wito wa mshikamano wa nchi za Kiislamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Muhammad Sarwat Ijaz Qadiri, kiongozi wa Harakati ya Sunni Pakistan, katika hotuba yake huku akisisitiza kuendelea kwa dhulma na ukatili kwa utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Palestina, na akaukosoa vikali Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kwa sababu ya ukimya na kutochukua hatua mbele ya mgogoro huu, na akasema: Taasisi hizi mbili, ambazo zinajinasibisha na ulinzi wa haki za binadamu, kwa ukimya wao zimeipa Israel ujasiri na uthubutu zaidi.

Akaongeza kwa kusema: Utawala wa Israel kila siku unawalenga watu wasio na ulinzi wa Ghaza kwa mashambulizi ya kikatili, na hakuna hifadhi yoyote katika eneo hili inayoweza kuwaokoka kutokana na mashambulizi na dhulma hizo. Vitendo hivi vinapingana na sheria zote za kimataifa za vita, na vinahesabiwa kuwa ni ukiukwaji wa wazi wa haki za binadamu na heshima ya mwanadamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha