Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, takriban asilimia 9 ya wakazi wa Ufaransa ni Waislamu, jambo linaloifanya kuwa nchi yenye jamii kubwa zaidi ya Kiislamu katika eneo la Ulaya Magharibi. Hata hivyo, kwa masikitiko makubwa, serikali ya Ufaransa mara kwa mara imekuwa ikichochea uhasama na vurugu dhidi ya Waislamu, na huendelea kushinikiza mbinu za kibaguzi na chuki dhidi ya Uislamu.
Pamoja na hayo, katika miezi ya hivi karibuni, kumekuwa na maandamano mengi ya raia nchini humo, yenye lengo la kulaani kila aina ya ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu. Vuguvugu hili la maandamano limechochewa zaidi na tukio la kuuawa kwa kijana Muislamu mwenye umri wa miaka ishirini kwa kushambuliwa na silaha kali ndani ya msikiti ulioko kusini mwa Ufaransa.
Mauaji hayo yalitokea mwishoni mwa mwezi Aprili, ambapo muuaji alimchukua video marehemu huku akitoa matamshi ya kibaguzi, na kisha kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii, jambo lililozua hasira kubwa kwa wananchi.
Viongozi wa jamii ya Wafaransa na mashirika ya kutetea haki za binadamu wametoa wito kwa serikali ya Ufaransa kuchukua hatua za haraka na madhubuti kukabiliana na ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu na kuenea kwa chuki dhidi ya Uislamu.
Chanzo: Shirika la Habari Karbala Now
Maoni yako