Jumapili 15 Juni 2025 - 21:13
Kusalia uislamu kunategemea suala la wilaya

Hawza / Mzungumzaji katika Haram tukufu ya Bibi wa Heshima, Bibi Maasuma (as), alisema kuwa Mwenyezi Mungu baada ya kutangaza wilaya ya Amirul-Mu’minin (as), alieleza: “Leo makafiri wamekata tamaa kwamba Uislamu utaondoka katika uso wa dunia.” Hii ni dalili kwamba kusalia kwa Uislamu kunategemea suala la wilaya, na wilaya ya kimungu kama ilivyokuwepo katika zama za Mtume (saw) na Maimamu (as), katika zama za ghaiba iko mikononi mwa Waliyyul-Faqih.

Shirika la Habari la Hawza - Ayatollah Shabzendedar alieleza kuwa uhai wa Uislamu unahusiana moja kwa moja na suala la wilaya, na akaongeza kuwa: “Wilaya kama ilivyokuwepo katika zama za Maimamu Maasumina (as), katika zama za ghaiba iko mikononi mwa Waliyyul-Faqih. Hivyo basi, leo hii uhai wa Uislamu umo mikononi mwa Kiongozi Mkuu, Ayatollah al-Udhma Khamenei (Mola amuhifadhi), na sisi tunaona jambo hili kwa uwazi katika siku hizi.”

Aliendelea kusema: “Mwenyezi Mungu Mtukufu kisha akasema kuwa: ‘Leo ambapo suala la wilaya limetangazwa, na Amirul-Mu’minin (as) ametangazwa kuwa ni Walii wa jamii ya Kiislamu, nimekukamilishieni dini yenu, na neema Yangu—ambayo ni neema ya uongofu, ufanisi, na kufikia kilele cha sa’adah na najat—nimeitimizia. Na nimeridhika kuwa Uislamu uwe ndiyo dini yenu.’”

Mzungumzaji katika Haram ya tukufu ya Bibi wa Heshima alitaja Aya ya 55 ya Surah An-Nur akasema: “Mwenyezi Mungu katika aya hii anatoa bishara kwa jamii ya Kiislamu kwamba wale wanaoamini na kutenda mema, Atawafanya kuwa makhalifa wake katika ardhi, na dini ambayo Amewachagulia Ataiimarisha katika ardhi, na baada ya waumini kuishi katika hali ya woga na mashaka kutokana na maadui, Atawapa usalama, utulivu na amani.”

Alibainisha kuwa: “Muumini mwenye kushikamana na wilaya, mbele ya matatizo ambayo maadui wamekusudia kuyasababisha leo, atasimama imara kama milima. Hatawahi kukata tamaa wala kuondoka katika uwanja wa mapambano, bali kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, atasimama katika uwanja huo, atapambana na maadui na atashuhudia nusra ya Mwenyezi Mungu.”

Ayatollah Shabzandahdar amesema: “Uhusiano wa Walii na Ummah ni sawa na uhusiano wa roho katika mwili wa mwanadamu. Ikiwa roho itatenganishwa na mwili, mwili utakuwa mzoga usio na harakati wala uhai. Hivyo basi, kile kinamchofanya mtu na jamii ya kibinadamu kuwa hai ni suala la wilaya. Tunapaswa kulithamini jambo hili, na kulihifadhi, ili Inshallah tuweze kushuhudia kudhihiri kwa Imam Mahdi (aj).”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha