Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, wakati ambapo Waislamu wa Uingereza walikuwa wakisherehekea Sikukuu ya Eid al-Adhha, ripoti mbalimbali ziliripotiwa kote nchini Uingereza zikihusu mashambulizi dhidi ya Waislamu nchini humo.
Haya yanajiri huku mchunguzi mmoja wa maoni ya wananchi wa eneo hilo akionesha kuwa Waingereza wengi wana mtazamo chanya au wa kutoegemea upande wowote kuhusu Waislamu.
Shirika moja limekadiria kuwa hasara iliyotokana na chuki dhidi ya Uislamu nchini Uingereza katika mwaka uliopita ilifikia kwa uchache paund milioni 243 (sawa na dola milioni 328.9), kiasi ambacho kinajumuisha gharama zinazohusiana na polisi, kuzuiwa na madai ya bima.
Kwa mujibu wa shirika hilo, kwa sasa Waislamu wengi wa Uingereza wanaamini kuwa hata katika uchunguzi na mwenendo wa haki, haki zao hupuuzwa.
Maoni yako