Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Maqsuud Ali Domki, Katibu Mkuu wa Idara ya Uchapishaji na Uenezi ya Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan, katika kongamano la maulamaa na masheikh wa Baluchistan, alilaani vikali jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya taifa lililodhulumiwa la Palestina, huku akieleza kuwa dhamira ya jamii ya kimataifa ambayo imeamka haiwezi tena kuvumilia dhulma hii ya wazi, na kwamba wakati umefika kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti na zenye athari.
Akiitaja hatua ya jeshi la utawala wa Kizayuni ya kuizuia meli ya misaada ya Ulaya kuwa ni uvunjaji wa wazi wa haki za kimataifa na misingi ya kibinadamu, alitoa wito kwa Umoja wa Mataifa, Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, na taasisi nyingine za kimataifa zenye mamlaka kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wa utawala huo.
Mwanazuoni huyu wa Kiislamu kutoka Pakistan, akizungumzia takwimu za kusikitisha za idadi ya wahanga wa Palestina, aliongeza kuwa: hadi sasa zaidi ya watu 54,000 wasio na hatia wameuawa kishahidi huko Palestina kwa mikono ya majeshi ya kigaidi ya wavamizi; jinai hizi zimeujeruhi sana uwepo wa mwanadamu.
Maoni yako