Jumatatu 9 Juni 2025 - 21:48
wilayat Faqihi ndio njia pekee inayodhamini utawala wa dini ya Uislamu na utekelezaji wa hukumu za Mwenyezi Mungu

Hawza/ Kile kinachojulikana leo kama "wilayat  Faqihi" katika muendelezo wa "wilaya ya Ahlul-Bayt (as)", ndio njia pekee inayoweza kudhamini utawala wa dini ya Uislamu na utekelezaji wa hukumu za Mwenyezi Mungu; kwa hivyo, ni lazima kuitetea kwa moyo na nafsi yote.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ali Abbasi, Rais wa J'amitul-Mustafa al-‘Alamiyya, katika kikao na kundi la wanafunzi kutoka Iraq wanaoshiriki kwenye kozi ya mafunzo ya muda mfupi na fursa za kielimu za J'amia hiyo, alitoa salamu za pongezi kutokana na mnasaba wa sikukuu za Eid al-Adh-ha na Ghadir na kusema:

“Sheria na majukumu yote ya Kiislamu yanategemea masilahi makubwa kwa Mwislamu binafsi na kwa Umma wa Kiislamu kwa ujumla.” Moja ya sheria hizo ni "Hija", ambayo kila mwaka makundi makubwa ya Waislamu huitekeleza, na bila shaka ibada hiyo kubwa imejengeka juu ya masilahi muhimu.

Aliendelea kusema kuwa: “Qur’an Tukufu inasema: ‘Mwenyezi Mungu ameifanya Baytullah al-Haram kuwa nguzo ya kusimama kwa Umma wa Kiislamu.’ Hii ina maana kwamba jukumu hili la kisheria lina umuhimu mkubwa kiasi kwamba ni nguzo ya Uislamu; bila hiyo, jamii ya Kiislamu huporomoka. Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaamrisha Waislamu kutoka pembe zote za dunia kukusanyika kuzunguka Nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa namna ambayo uimara na heshima ya Umma wa Kiislamu umefungamanishwa na jambo hilo.”

Rais wa J'amiatul-Mustafa alisisitiza umuhimu wa kutumia fursa ya Hija kwa ajili ya kulinda heshima na uimara wa dunia ya Kiislamu, na akasema: “Leo tunashuhudia kuwa Waislamu katika maeneo mbalimbali, hasa katika eneo letu hili, wamekumbwa na matatizo mengi. Msimu wa Hija ungebidi kuwa fursa ya kuyatatua matatizo haya, lakini kwa masikitiko makubwa fursa hiyo haitumiki ipasavyo.”

Akiashiria kuanzishwa kwa mamia ya vituo vya kidini vya kifahari na baadhi ya serikali za Kiislamu, huku serikali hizo hizo zikiendelea kuwa na uhusiano mpana wa kiuchumi na utawala wa Kizayuni unaolaaniwa, alisema: “Hili linaonyesha kuwa hatujatumia kikamilifu uwezo wa kiibada, kisiasa na kijamii wa ibada ya Hija.”

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Abbasi alieleza kuwa, sababu ya kukosa faida kutoka katika fursa hizi ni kujiweka mbali na mhimili wa "wilaya" na "Ghadir", na akasisitiza kuwa:
“Ninyi wapendwa, ambao mnashughulika katika maeneo mbalimbali kusambaza na kueneza maarifa ya Kiislamu na Kimungu, mnajua vyema kuwa msingi mkuu katika nguzo zote za Uislamu ni "wilaya"; na kwamba mihimili mingine yote hupata maana kutoka katika msingi huu.”

Aliendelea kusema: “Kile kinachojulikana leo kama "wilayat Faqihi, ambayo ni muendelezo wa "wilaya ya Ahlul-Bayt (as)", ndio njia pekee inayoweza kudhamini utawala wa dini ya kiislamu na utekelezaji wa hukumu za Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, ni lazima kuilinda na kuitetea kwa moyo wote.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha