Jumamosi 31 Mei 2025 - 09:13
Kuvumilia wahalifu kunapelekea kuvunjika kwa jamii

Dkt. Muhammad Tahir-ul-Qadri, Kiongozi wa Harakati ya Minh'aj al-Qur’an Pakistan, katika kikao cha kielimu kilichofanyika Manchester Uingereza, kwa kusisitiza heshima ya uhai wa binadamu, alilitaja kosa la mauaji ya kiholela katika mtazamo wa Uislamu kuwa ni dhambi isiyosameheka, na akasema: "Muuaji hata harufu ya Pepo hataisikia."

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Dkt. Muhammad Tahir-ul-Qadri, mwanzilishi na kiongozi wa Harakati ya Minh'aj al-Qur’an Pakistan, katika kikao cha kielimu na kifikra kilichohudhuriwa na maulamaa na wahubiri katika mji wa Manchester Uingereza, katika hotuba yake, alisisitiza umuhimu wa kulinda heshima ya uhai wa binadamu. Alitaja mauaji ya kiholela kwa mujibu wa Sheria ya Kiislamu kuwa ni dhambi kubwa isiyosameheka na yenye kwenda kinyume na mfumo wa kimaumbile wa maisha ya binadamu uliowekwa na Mwenyezi Mungu, pia lisisitiza kuwa: "Muuaji hata harufu ya Pepo hataisikia."

Aliendelea kwa kusisitiza juu ya wajibu wa kidini na kimaadili wa maulamaa, makhatwibu na wahubiri wa dini na akasema: "Kuielimisha jamii juu ya heshima ya uhai wa binadamu na kufafanua hatari na madhara yatokanayo na uhalifu wa mauaji ni miongoni mwa majukumu makuu ya wasomi wa dini. Jamii inapaswa kuwa makini dhidi ya maovu kama vile mauaji ya kiholela na ichukue msimamo wa wazi dhidi yake."

Mwanafikra huyo wa Kiislamu alibainisha kuwa: "Katika Sheria tukufu ya Kiislamu, mauaji ya kiholela, iwe kwa mwislamu au asiye mwislamu, yamekataliwa vikali na ni miongoni mwa madhambi makubwa zaidi. Mtume Mtukufu wa Uislamu (saw) amesema: ‘Muuaji hata harufu ya Pepo hataisikia.’"

Akaongeza: "Muuaji hamuui tu mtu mmoja, bali anavuruga mfumo wa maisha ya binadamu uliowekwa na Mwenyezi Mungu na anavuruga utaratibu mtukufu ambao Mwenyezi Mungu ameuweka katika huu ulimwengu."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha