Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Muhammad Amin Shahidi, Mwenyekiti wa Umoja wa "Umma Moja Pakistan", akijibu kauli za hivi karibuni za Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Shahbaz Sharif, kuhusu kuunga mkono mpango wa nyuklia wa amani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika tamko lake, ameukaribisha msimamo huo na kuutambua kama unaoakisi matakwa ya taifa la Pakistan.
Amesisitiza kwamba kunufaika na teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani na kwa misingi ya mafundisho ya Kiislamu ni haki halali na isiyokanushika kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akaongeza kusema: Kufaidika na nishati ya nyuklia na kuwa na uwezo wa kujilinda ni haki isiyopingika kwa kila taifa linalokabiliana na vitisho vikubwa dhidi ya usalama na mamlaka yake. Kama ambavyo Jamhuri ya Kiislamu ya Pakistan, kulingana na mazingira yake ya kiusalama, imefanikiwa kupata nguvu ya nyuklia, vivyo hivyo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia ina haki ya kutumia teknolojia ya nyuklia ya amani kwa ajili ya kutimiza mahitaji yake ya kitaifa.
Maoni yako