Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei alijibu swali la kifiqhi kuhusu “kuwajibu wanaotoa matusi,” ambalo linawasilishwa kwa wahusika wanaopenda masuala haya.
"Kuwajibu wanaotoa matusi"
Swali:
Je, kujibu mtu anayetoa matusi na kumrudishia kile kile alichokisema kuna shida yoyote?
Jawabu:
Kujibu matusi kwa mwenye kutoa matusi kwa mtazamo wa kulipiza kisasi (taqāṣ) hakuna shida kwa sharti mbili:
Sharti la kwanza:
Matusi yanayorudishwa yawe sawa na yale aliyoyasema, si zaidi wala makali kuliko hayo.
Sharti la pili:
Maneno hayo yasihusishe haramu nyingine yoyote.
Maoni yako