Jumanne 29 Aprili 2025 - 20:45
Dhana na historia ya Ghaiba (kutoweka)

Ghaiba au maisha ya kifichoni si jambo jipya lililotokea kwa mara ya kwanza tu kuhusu hujjah wa mwisho wa Mola Mlezi, bali kutokana na riwaya nyingi inaonekana kwamba baadhi ya Manabii wakubwa wa Mwenyezi Mungu walikuwa na sehemu ya maisha yao katika hali ya maficho au ghaiba. Na jambo hili lilitokea kutokana na hekima pamoja na maslahi ya Kimungu, wala si matakwa binafsi au kwa maslahi ya kifamilia.

 Shirika la Habari la Hawza- Jambo la kwanza la kuzungumzwa ni kwamba "ghaiba" maana yake ni "kuwa mafichoni kutokana na uono wa watu", na wala si kutokuwepo kabisa; kwa hivyo katika sehemu hii, tunazungumzia kipindi ambacho Imamu Mahdi (a.s) yupo mafichoni, watu hawawezi kumuona, ilhali yeye yupo kati yao na anaishi miongoni mwao. Ukweli huu umeelezwa katika riwaya za Maimamu Maasum (a.s) kwa maneno mbalimbali.

Imamu Ali (a.s) alisema:

 
«فَوَ رَبِّ عَلِیٍّ إِنَّ حُجَّتَهَا عَلَیْهَا قَائِمَةٌ مَاشِیَةٌ فِی طُرُقِهَا دَاخِلَةٌ فِی دُورِهَا وَ قُصُورِهَا جَوَّالَةٌ فِی شَرْقِ هَذِهِ اَلْأَرْضِ وَ غَرْبِهَا تَسْمَعُ اَلْکَلاَمَ وَ تُسَلِّمَ عَلَی اَلْجَمَاعَةِ تَرَی وَ لاَ تُرَی إِلَی اَلْوَقْتِ وَ اَلْوَعْدِ》

Naapa kwa jina la Mola wa Ali, hakika hoja wa umma yupo imara, anatembea mitaani mwao, anaingia majumbani mwao na katika makasri yao, anazunguka mashariki na magharibi mwa ardhi hii, anasikia maneno ya watu, anayasalimu makundi yao, anaona lakini haonekani mpaka wakati na ahadi yake ifike. (Ghaibat Nuuman، uk. 144)

Aina nyingine ya ghaiba pia imeelezwa kumuhusu yeye.

Imamu Swadiq (a.s) alisema:


«إِنَّ فِی صَاحِبِ هَذَا اَلْأَمْرِ سُنَناً مِنَ اَلْأَنْبِیَاءِ عَلَیْهِمُ السَّلاَمُ ... وَ أَمَّا سُنَّتُهُ مِنْ یُوسُفَ فَالسِّتْرُ یَجْعَلُ اَللَّهُ بَیْنَهُ وَ بَیْنَ اَلْخَلْقِ حِجَاباً یَرَوْنَهُ وَ لاَ یَعْرِفُونَهُ»

Hakina pana kwa mwenye jambo hili suna za Manabii (a.s) … na kuhusu sunna yake kutoka kwa Yusuf ni kufichika; Mwenyezi Mungu ataweka baina yake na viumbe kizuizi, watu watamwona lakini hawatamtambua. (Kamalu-d'in، juz. 2, uk. 350)

Kwa hiyo, kuhusu Hadhrat Mahdi (a.s) khaiba hutafsirika kwa aina mbili: aina ya kwanza haonekani kabisa katika macho ya watu, na nyingine anaonekana lakini hatambuliki. Lakini katika hali zote, yeye yupo miongoni mwa watu.

Historia ya Ghaiba (kutoweka)

Ghaiba na maisha ya kifichoni si jambo jipya lililotokea kwa mara ya kwanza tu kumhusu hoja wa mwisho wa Mola Mlezi, bali kutokana na riwaya nyingi inaonekana kwamba baadhi ya Manabii wakubwa wa Mwenyezi Mungu ilikuwa sehemu ya maisha yao ni mafichoni na katika khaiba. Na hili lilikuwa kutokana na hekima na maslahi ya Kimungu, wala si kwa sababu ya matakwa binafsi au maslahi ya kifamilia.

Kwa hivyo, ghaiba ni miongoni mwa (desturi za Kimungu) ambazo zilitokea katika maisha ya Manabii kama Idris, Nuh, Swalih, Ibrahim, Yusuf, Musa, Shuayb, Ilyas, Sulaiman, Daniyal na Isa (a.s). Na kila mmoja wa wajumbe hao wa Mwenyezi Mungu, kulingana na mazingira yake, alikaa miaka kadhaa katika ghaiba (maficho).

Ndiyo maana katika riwaya, ghaiba ya Imamu Mahdi (a.s) imeelezwa kuwa ni miongoni mwa sunnah za Manabii, na mojawapo ya sababu za ghaiba yake ni utekelezaji wa sunna za Manabii (a.s) katika maisha yake.

Imamu Swadiq (a.s) anasema:


«إِنَّ لِلْقَائِمِ مِنَّا غَیْبَةً یَطُولُ أَمَدُهَا؛» 


Hakika ana al-Qa'im (Imam Mahd) miongoni mwetu kuna ghaiba ambayo muda wake utakuwa mrefu.

«فَقُلْتُ لَهُ وَ لِمَ ذَاکَ یَا اِبْنَ رَسُولِ اَللَّهِ؟»  


Nikamuuliza: Ni kwa nini hivyo, ewe mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu?

«.قَالَ إِنَّ اَللَّهَ عَزَّ وَ جَلَّ أَبَی إِلاَّ أَنْ یُجْرِیَ فِیهِ سُنَنَ اَلْأَنْبِیَاءِ عَلَیْهِمُ السَّلاَمُ فِی غَیْبَاتِهِمْ»


Akasema: Hakika Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla, amekataa isipokuwa zitekelezwe ndani yake suna za Manabii (a.s) katika ghaiba zao. (Ilalu-Sharaii, juz. 1, uk. 245)  

Katika maneno haya, pia inadhihirika kwamba suala la ghaiba ya Imamu Mahdi (a.s) lilishazungumzwa miaka mingi kabla ya kuzaliwa kwake, na viongozi wa Kiislamu kuanzia Mtume Muhammad (s.a.w) hadi Imamu Hasan al-Askari (a.s) walikuwa wakielezea kuhusu ghaiba yake, baadhi ya sifa zake, na matukio yatakayotokea wakati wa ghaiba, na pia walielekeza majukumu ya waumini wakati huo.

Mtume Muhammad (s.a.w) pia alisema kuhusu ghaiba Imamu Mahdi (a.s):

 
«اَلْمَهْدِیُّ مِنْ وُلْدِی اِسْمُهُ اِسْمِی وَ کُنْیَتُهُ کُنْیَتِی أَشْبَهُ اَلنَّاسِ بِی خَلْقاً وَ خُلْقاً تَکُونُ بِهِ غَیْبَةٌ وَ حَیْرَةٌ تَضِلُّ فِیهَا اَلْأُمَمُ ثُمَّ یُقْبِلُ کَالشِّهَابِ اَلثَّاقِبِ یَمْلَؤُهَا عَدْلاً وَ قِسْطاً کَمَا مُلِئَتْ جَوْراً وَ ظُلْماً

“Mahdi ni miongoni mwa watoto wangu. Jina lake ni jina langu, na kunia yake ni kunia yangu. Yeye ndiye anayefanana nami zaidi kwa umbo na tabia. Itakuwa kwake ghaiba na shaka, umma utapotea, kisha atatokea kama nyota ing’arayo kwa nguvu, na ataijaza dunia uadilifu na haki kama ilivyokuwa imejaa dhulma na uonevu.”  (Kamalu- D'in، juz. 1, uk. 286)

Utafiti huu unaendelea...
Imenukuliwa kutoka katika kitabu «Negin Afarinesh» huku ikifanyiwa mabadiliko kiasi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha