Alhamisi 27 Novemba 2025 - 13:00
Jiji la Nairobi Lawa Mwenyeji wa Maonesho Maalumu ya Sanaa kwa Vijana wa Kenya 2025

Hawza/ Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupitia Baraza lake la Utamaduni umetangaza rasmi kufanyika Maonesho ya sanaa mahsusi kwa vijana wa Kenya 2025, yatakayofanyika kuanzia tarehe 1 hadi 5 Desemba 2025 jijini Nairobi.

Kwa mujibu wa Shirika la Shirika la Habari la Hawza, maonesho hayo yatafanyika kila siku kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa 10:30 jioni, yakilenga kuibua na kukuza vipaji vya kisanaa miongoni mwa vijana, sambamba na kuwawezesha kiuchumi kupitia uuzaji wa kazi zao za sanaa.

Baraza la Utamaduni limewahamasisha wananchi, wadau wa sanaa na taasisi mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika tukio hilo ili kuwaunga mkono vijana wenye vipaji kwa kutazama, kuthamini na kununua kazi zao bora na za kuvutia za sanaa.

Hafla ya utoaji wa tuzo

Aidha, hafla ya utoaji wa tuzo kwa washiriki bora imepangwa kufanyika tarehe 5 Desemba 2025, kuanzia saa 9:00 alasiri, katika jengo la Parklands Plaza, Ghorofa ya 7, Chiromo Lane, eneo la Westlands.

Waandaaji wamesisitiza kuwa ushiriki kwa wingi ndio chanzo cha hamasa, motisha na matumaini mapya kwa kizazi kijacho cha wasanii wa Kenya, huku wakitoa wito kwa wananchi kutokosa tukio hili muhimu la kisanaa.

Jiji la Nairobi Lawa Mwenyeji wa Maonesho Maalumu ya Sanaa kwa Vijana wa Kenya 2025

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha