Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Habari wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Iraq, Ayatullah A‘rafi katika Kongamano la Kimataifa la Mtafiti Mirza Naa’ini huko Najaf al-Ashraf, lililofanyika katika Ukumbi wa Alawi wa Jumuia ya Alawi katika mji wa Najaf al-Ashraf, likihudhuriwa na shakhsia za kielimu, alifafanua sifa kuu za shakhsia ya Mirza pamoja na nafasi na mchango wake wa kielimu, kijamii na kisiasa, na akasisitiza nafasi yake ya pekee katika historia ya hawza.
Mkurugenzi wa Hawza baada ya kutoa pongezi za kuwakaribisha wahudhuriaji, wageni wa kongamano, wanachuoni, pamoja na wawakilishi wa nyumba za marjaa wakubwa wa taqlidi huko Najaf al-Ashraf na Qum, na pia nyumba ya Imam aliye fariki (Quddisa Sirruh), na ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran, na nyumba ya Ayatullah al-‘Udhma Sistani pamoja na ofisi zake huko Najaf na Qum, na hasa Ataba Tukufu ya Alawi na Ataba Tukufu ya Husayni, na Katibu Mkuu wa Kongamano, na nyumba ya Ayatullah Naa’ini pamoja na washiriki wote wa kongamano, na kutoa shukrani za pekee kwa uungaji mkono wa Ayatullah Sistani katika kuandaliwa kongamano, na kadhalika… alisisitiza juu ya nukta hii kwamba kufanyika kwa makongamano ya aina hii, sambamba na kutoa heshima na kuzitambulisha shakhsia kubwa za hawza na shakhsia za fikra na islah katika historia ya Uislamu na Ushia, kutachangia pia kuitambulisha hawza, katika kizazi kipya na kwenye vyuo vikuu.
Aidha alisema: Vilevile, kutaimarisha zaidi misingi ya utambulisho wa Kiislamu na wa kihawza ndani ya hawza na katika jamii ya kielimu. Pia makongamano kama haya yatakuwa chanzo cha msukumo kwa vizazi vipya vya wanahawza, kwa kuwa yatawatambulisha, na jihadi na mapambano ya wanachuoni wa hawza katika nyanja za elimu, jihadi ya kijamii na kisiasa, na yatakuwa kama taa inayoangaza njia ya wanahawza kuelekea mustakabali mwema na wenye mwangaza.
Maoni yako