Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, baada ya utawala bandia wa Kizayuni kuanzisha mauaji ya halaiki huko Ghaza na kufanya vita mfululizo dhidi ya watu wa maeneo kama Ukingo wa Magharibi, Lebanon, Yemen, Iran na Syria, ulihitaji kuongeza idadi ya wanajeshi wake. Lakini kushindwa kufanya hivyo kuliifanya serikali ya Netanyahu iingie katika hali ya kuyumba vibaya, hadi kufikia kwamba katika mpango wa hivi karibuni wa Marekani, ilikuwa ikiomba kupelekwa washauri wa kijeshi wa Kimarekani huko Ghaza.
Wakati ambapo, kwa mujibu wa propaganda za utawala huo haramu wa Kizayuni, inatarajiwa kuwa wanaume na wanawake wengi Wayahudi watumikie jeshini kwa takriban miaka miwili, kuna kundi ambalo daima limekuwa likipewa msamaha—Wayahudi wa orthodox wanaojulikana kama Haredim.
Mwezi Juni 2024, Mahakama ya Juu ya Israel ilitoa uamuzi kwamba wao pia wanaweza kulazimika kuingia jeshini, jambo lililozua upinzani mkubwa miongoni mwa Haredim.
Mwezi uliopita, mamia ya maelfu ya wanaume wa Haredi waliijaza Jerusalem yote katika moja ya maandamano yao makubwa yaliyotambuliwa kama maandamano ya Ultra-Orthodox. Tukio hili linaonesha vyema mtikisiko wa serikali ya Netanyahu na kuvunjika kwa muundo wa kisiasa wa Israel.
Chanzo: Middle East Eye
Maoni yako