Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari Hawza, Hujjatul-Islam Sheikh Ahmad Qablan, Mufti wa juu wa Ja‘fariyya na mwanachuoni mashuhuri wa Lebanon, katika tamko lake amelaani shambulio la jinai la jeshi la Kizayuni huko Dhahia kusini, ambalo lililenga moyo wa uamuzi wa kitaifa wa Lebanon, yaani serikali na uwepo wake.
Amesisitiza kuwa; visingizio havikubaliki, bali kile kinachohitajika ni jibu rasmi na la kitaifa lenye uzito unaolingana na wazimu huu wa Kizayuni. Serikali ya Lebanon imelazimika kujitokeza katika kiwango cha mdhamini wa usalama wa taifa, siyo kulaani kwa maneno matupu. Uvamizi huu wa kishenzi wa Kizayuni hautabadili kitu isipokuwa kutuimarisha zaidi katika kushikamana na chaguo letu la kitaifa na la kiudhibiti.
Sheikh Qablan amesema: Hakuna mdhamini wa kuitetea nchi hii isipokuwa jeshi, taifa, muqawama, umoja wa kitaifa na sera za kiudhibiti zinazostahili familia ya Lebanon. Sasa ni wakati wa kusisitiza maslahi makuu ya Lebanon mbele ya hatari kubwa zaidi ya Kizayuni inayotishia asili ya uwepo wa Lebanon.
Maoni yako