Jumanne 25 Novemba 2025 - 20:38
Utukufu wa ibada ya Bibi Zahraa (a.s) Kulingana na Mtazamo wa Ayatullah A-Udhma Javadi Amoli

Hawza/ Ayatullah Javadi Amoli amebainisha kuwa: Bibi Zahraa (a.s) alipokuwa akisimama kuswali alikuwa akijikita kiasi kikubwa kwenye utukufu wa Mwenyezi Mungu na kupotea kabisa katika jalali ya Mola, kiasi cha kwamba pumzi zake zilikuwa zikimwishia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Javadi Amoli katika maelezo yake aligusia nafasi ya kiibada ya Bibi Zahraa (a.s) na kusema kwamba: Bibi Zahraa (a.s) alipokuwa akisimama kuswali alikuwa akizamia mno katika utukufu wa Mwenyezi Mungu na kupotea kabisa katika jalali ya Mola Mtukufu kiasi kwamba pumzi zake zilikuwa zikipungua.
“Na Fatima (a.s) alikuwa akivuta pumzi kwa shida wakati wa kuswali kwa sababu ya kumwogopa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.” [1]

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kuhusiana ibada ya Fatima (a.s) alikuwa akisema:

“Wakati Zahraa anaposimama katika mihrabu ya ibada, hung'aa kwa malaika wa mbinguni kama nyota; na Mwenyezi Mungu huwaambia malaika: Enyi malaika! Mtazameni mja wangu bora kabisa, Fatima. Yeye anasimama mbele Yangu na mwili wake wote unatetemeka kwa kuniogopa, na kwa unyenyekevu kamili wa moyo ananiabudu.” [2]

[1] Bihar al-Anwar, juz. 67, uk. 400
[2] Bihar al-Anwar, juz. 43, uk. 172
Fatima (a.s), ni kielelezo cha ubinadamu

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha