Jumanne 29 Aprili 2025 - 20:28
Mgogoro wa Parachinar nchini Pakistan bado unaendelea kugharimu maisha; magaidi hawana huruma hata kwa watoto

Kufuatia kuendelea kuzingirwa watu wa Parachinar kwa kipindi cha miezi kadhaa, kikao muhimu kimefanyika mjini Islamabad huku kikhudhuriwa na kundi la wanazuoni, pamoja na watu mashuhuri wa kisiasa na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha  Shirika la Habari la Hawza,, kikao hiki muhimu kilifanyika mjini Islamabad kutokana na kuendelea kuzingirwa takriban miezi kadhaa katika eneo la Parachinar. Washiriki katika mkutano huo, walielezea wasiwasi wao kuhusu hali mbaya inayowakumba watu wa eneo la Kuram, walitaka vizuizi hivyo vikomeshwe mara moja na hali ya usalama na utulivu irejee katika eneo hilo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha