Jumamosi 26 Aprili 2025 - 08:22
Khums ya mauzo ya zawadi na urithi

Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi amejibu istiftaa kuhusu “Khums ya mauzo ya zawadi na urithi.”

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Hdhrat Ayatollah al-Udhma Khamenei amejibu istiftaa kuhusu “Khums ya mauzo ya zawadi na urithi” jawabu ambalo linawasilishwa kwa wafuatiliaji kama ifuatavyo:

Khums ya mauzo ya zawadi na urithi

Swali: Nilikuwa na kipande cha ardhi ambacho kilikuwa zawadi kutoka kwa baba yangu, na baada ya muda nilikiuza. Je, fedha ya mauzo ya ardhi hiyo inapaswa kutolewa khums?

Jawabu: Ardhi hiyo yenyewe wakati wa kupewa zawadi haina khums. Lakini ongezeko la thamani ya ardhi hiyo, ikiwa ardhi hiyo ilihifadhiwa kwa nia ya kuongezeka thamani au kwa ajili ya kuuza na kununua, basi kwa mujibu wa tahadhari ya wajibu, baada ya kutoa kiasi kilichozidi, hujumuishwa katika mapato ya mwaka ambao ardhi imeuzwa. Endapo kiasi hicho kitapita hadi mwisho wa mwaka wa khums bila kutumika, basi kitakuwa na khums. Vinginevyo, ongezeko hilo la thamani halitapasa na khums.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha