Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Imam Swadiq (a.s) anaonyesha kushangazwa na makundi manne ya watu kwa nini, wakati wa dhiki na matatizo, hawakimbilii kwenye dhikri nne zilizo na uzoefu na zinazotoa tiba.
Dhikri hizi ni kama ifuatavyo:
1. Wakati wa hofu, wasiwasi na mashaka: Dhikri Tukufu:
"حسبنا الله ونعم الوكيل"
“Tosha yetu ni Mwenyezi Mungu, na ni bora ya tegemezi.”
2. Wakati wa huzuni na masikitiko:
Dhikri Tukufu:
"لا اله الا انت سبحانك اني كنت من الظالمين"
“Hakuna Mola isipokuwa Wewe, Umetakasika, hakika mimi ni miongoni mwa wenye kujidhulumu.”
3. Wakati kuna hofu ya kudanganywa au kufanyiwa hila:
Dhikri Tukufu:
"افوض امري الى الله ان الله بصير بالعباد"
“Namkabidhi Mwenyezi Mungu jambo langu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja.”
4. Kwa ajili ya kuomba riziki halali:
Dhikri Tukufu:
"ما شاالله لا حول ولا قوة الا بالله"
“Alitakalo Mwenyezi Mungu litakuwa; hakuna nguvu wala uwezo isipokuwa kwa [msaada wa] Mwenyezi Mungu.”
Maoni yako