Jumatano 23 Aprili 2025 - 16:39
Mtu ambaye ana matatizo na jamii, basi aimarishe mafungamano kati yake na Mwenyezi Mungu

Ayatollah Jawadi Amuli amesema: Mtu ambaye ana matatizo kwenye jamii na anataka kuboresha uhusiano kati yake na watu wengine, ni lazima aimarishe na kupendezesha uhusiano wake na Mwenyezi Mungu. Kwa sababu funguo za nyoyo za watu ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Jawadi Amuli katika maandishi yake amezungumzia mada ya “Kuboresha mafungano na Mungu” na akasema: Amiril-M'uminina (a.s) amesema:

«مَنْ أصْلح ما بینه وَبین الله، أصْلح الله سُبحانَه وتعالی ما بینه وَبین النّاس.»

“Yeyote atakae tengeneza uhusiano kati yake na Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamtengenezea uhusiano kati yake yeye na watu wengine.”


Hadithi hii yenye nuru inahusiana na masuala ya kijamii; mtu ambaye ana matatizo katika jamii na anataka kuboresha uhusiano kati yake na watu wengine, ni lazima aimarishe na kupendezesha uhusiano wake kati yake na Mwenyezi Mungu. Kwa sababu funguo za nyoyo za watu ziko mikononi mwa Mungu, na sharti la kuboreka kwa mahusiano kati yake na wengine ni kuboresha uhusiano wake kati yake na Mwenyezi Mungu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha