Jumanne 22 Aprili 2025 - 10:33
Raia wa Bahrain ametoa hadia nakala ya maandishi iliyo na thamani kubwa kwenye Haram ya Imamu Husein (a.s)

Hawza; Nakala hii ya kipekee ya Qur'ani Tukufu iliyohifadhiwa kwa maandishi ya mkono ina urefu wa mita 1,250, na imetolewa kama zawadi kuielekea Haram ya Imamu Husein (a.s).

Shirika la Habari la Hawza; Kazi hii ya kipekee isiyo na kifani, ambayo imefanywa kwa ustadi mkubwa wa kisanaa na bidii isiyo ya kawaida, inaonesha uhusiano na mapenzi ya kina ya mtoaji juu ya Ahlul-Bayt (a.s).

Wakati wa hafla ya utoaji wa kazi hii ya kisanii na yenye thamani kubwa, Sheikh Abdulmahdi al-Karbalai, mwakilishi wa Ayatollah Sistani, alimpongeza mwana sanaa huyu mashuhuri na kulisifu tukio hili la kuvutia kuwa ni alama ya umoja wa kiislamu na kiunganishi cha kudumu miongoni mwa wapenzi wa Ahlul-Bayt (a.s).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha