Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, tangia kuanza kwa vita vya Ghaza hadi sasa, waandishi wa habari na wapiga picha walioko katika ukanda huo wamekuwa na nafasi muhimu katika kuwaamsha watu duniani na kufikisha taarifa kuhusu jinai ambazo kila siku zinawakumba watu wa Ghaza. Kwa sababu hii, waandishi wa habari na wapiga picha wameingizwa kwenye orodha ya walengwa na maadui wa Kizayuni.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa hadi sasa, zaidi ya watu 200 wanao husika na sekta ya habari wameuawa kishahidi na utawala wa Kizayuni.
Fatma Hassouneh, binti wa makamo wa Kipalestina ambaye kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu alikuwa akipiga picha zinazo akisi maumivu na masaibu yanayo wapata watu wa Ghaza katika vita hiyo, aliuawa kishahidi katika mashambulizi ya mabomu katika Ukanda wa Ghaza akiwa pamoja na familia yake.
Habari za kuuawa kishahidi kwa Fatma Hassouneh zilitangazwa punde tu baada ya kutangazwa kushiriki katika filamu ya maisha yake yenye kichwa cha habari kisemacho "Weka nafsi yako mkononi mwako kisha tembea" katika tamasha la Cannes.
Maoni yako