Ijumaa 18 Aprili 2025 - 14:33
Je, Qur’ani Tukufu imewataja Wayahudi kuwa ni watu bora kuliko wengine?

Qur’ani Tukufu imewapa Bani Isra’il daraja ya juu katika wakati wao kwa sababu ya neema walizopewa na Mwenyezi Mungu. Ubora huu ulikuwa wa muda maalumu na hali mahususi, na hauwahusishi Bani Isra’il wote katika historia nzima, bali unawahusu wafuasi wa dini ya Kiyahudi katika kipindi ambacho wa dini hiyo ilikuwa na nafasi. Ukiachilia mbali Bani Isra’il, Qur’ani pia imewateua watu na makundi mengine kuwa bora ulimwenguni.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Qur’ani Tukufu imewapa Bani Isra’il daraja ya juu katika kipindi chao kwa sababu ya neema walizopewa na Mwenyezi Mungu. Ubora huu ulikuwa wa muda maalumu, na haukuwahusisha Bani Isra’il wote katika historia nzima, bali uliwahusu wafuasi wa dini ya Kiyahudi katika kipindi ambacho wa dini hiyo ilikuwa ikizingatiwa. Ukiachilia mbali Bani Isra’il, Qur’ani pia imewateua watu na makundi mengine kuwa bora ulimwenguni.

Swali:  
Je, Qur’ani inawahesabu Mayahudi kuwa ni taifa bora?  
Je, aya hii ni ushahidi wa ubora wa Wayahudi?  
(“Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni neema zangu nilizo kuneemesheni, na nikakuteuweni kuliko wote wengineo..”)

Jibu:  
Dini zote za Mwenyezimungu katika zama zake zilikuwa ni njia bora na salama zaidi ya kuufikia uokovu. Hivyo basi, wafuasi wa dini hizo nao walihesabiwa kuwa miongoni mwa watu bora zaidi. Katika baadhi ya aya za Qur’ani, Bani Isra’il wametajwa na Mola wao kwa maneno haya:[1]
“Enyi Bani Isra’il! Kumbukeni neema zangu ambazo Niliwaneemesga, na Niliwafadhilisha juu ya walimwengu,”(wa zama zenu).[2]
Na ubora huu umetajwa pia kwa kauli ya Nabii Musa (a.s), ambapo alisema:  
“Je, niwe nikiwatakia mungu mwingine asiye kuwa Mwenyezi Mungu (ambaye hastahili kuabudiwa)? Hali ya kuwa Yeye ndiye aliyewafadhilisha juu ya walimwengu (wa kipindi chenu).”[3]

Katika aya hizi kuna mambo yanayohitaji ufafanuzi zaidi. Kwanza, ni neema gani ambazo Mwenyezi Mungu aliwapa? Pili, nini maana ya kuwapa ubora juu ya walimwengu?..

Katika hili, tunasema kwamba Mwenyezi Mungu katika aya nyingine ameonyesha mifano ya neema zake kwa Bani Isra’il:  
“Na kwa yakini tuliwapa Bani Isra’il Kitabu na Ufalme na Unabii, na tukawaruzuku vilivyo vya halali, na tukawafadhilisha juu ya walimwengu (wa zama zao).”[4]

Neema nyingi nyingine pia walipewa Wayahudi; kutoka kwenye neema ya uongofu na imani, hadi ukombozi kutoka mikononi mwa Firauni na kupata tena heshima na uhuru wao![5] Na vilevile kula chakula maalum cha mbinguni,[6] Qur’ani imesimulia visa vingi kuhusu neema hizi.

Kutokana na haya, baadhi ya wafasiri wa Qur’ani wanaona kuwa uwepo kwa manabii wengi miongoni mwa Bani Isra’il kuwa ni fadhila kwao;[7] kwani bila shaka uwepo wa watu wengi wema katika jamii huleta athari chanya, huongeza mwelekeo wa kumcha Mungu, na huchangia kuwapa ubora wa jamii ile kuliko nyengine.

Kwa upande mwingine, hata kama tutakubali kwamba Bani Isra’il walikuwa bora kwa maana pana, baada ya kipindi cha Nabii Isa (a.s) kwa kuwa yeye na wafuasi wake wengi walikuwa miongoni mwao, lakini Ahul-kitabu baada ya uislamu hawahusiki tena na ubora huo. Kwa sababu licha ya kuwa hawana ubora juu ya binadamu wengine, bali wanalaumiwa kwa kutoifuata risala ya Mtume Muhammad (s.a.w), na wengi wao wako mbali na uongofu. Kwa msingi huu, fadhila iliyotajwa inawahusu Wayahudi wa nyakati za zamani.

Ni muhimu kutambua pia kwamba kauli ya “Niliwafadhilisha juu ya walimwengu” haimaanishi binadamu wote katika historia nzima, bali ni dhahiri kuwa inawahusu tu wale wajukuu wa Nabii Ya’qub (a.s) waliokuwa wakiifuata dini ya Kiyahudi katika kipindi ambacho ilikuwa ndio dini ya haki.[8] Sio wale Bani Isra’il ambao Qur’ani imewataja kwa maneno haya:  
“Wale ambao Mwenyezi Mungu amewalaani, na amewaghadhibikia, na baadhi yao aliwageuza kuwa nyani na nguruwe, na wanaoabudu masanamu hao ndio waovu kabisa na walio mbali na njia iliyo sawa.”[9][10]

Sababu zingine zinazoonyesha kuwa ubora huu haukuwa wa milele wala kwa kila mmoja ni:

1. Kuna aya zinazoonesha kuwa Waislamu ni umma bora zaidi kwa wanadamu:  
“{ كُنتم خَیرَ أُمَّةٍ أُخرجت لِلنَّاسِ... }

2. Hakika Bani Isra’il hawana ubora juu ya Yaaqub (Isra’il mwenyewe), wala juu ya Is’haaq na Ibrahimu.

2. Katika Qur’ani, si Bani Isra’il tu waliotajwa kuwa bora, bali watu na makundi mengine pia wametajwa:  
“Hakika Mwenyezi Mungu amemteua Adam, na Nuh, na jamaa ya Ibrahimu, na jamaa ya Imran juu ya walimwengu.”[12]
“Na Ismail, na Alyasa’, na Yunus, na Lut wote tumewafadhilisha juu ya walimwengu.”[13]

Kwa hiyo, kama tukitafsiri kauli ya “Niliwafadhilisha juu ya walimwengu” kwa Bani Isra’il kuwa ni ubora juu ya binadamu wote, basi itazuka mgongano na aya hizi nyingine.

Hatimaye, ni muhimu kufahamu kuwa kuwa bora na kuchaguliwa na Mungu kunaleta matarajio makubwa. Kwa hivyo tunaona kwamba katika aya nyingi, Mwenyezi Mungu amewalaumu na kuwakemea zaidi kuliko watu wengine kwa sababu ya makosa yao.

Rejea:
1. Katika aya hii na aya zinazofanana nayo, neno “Bani Isra’il” linawahusu Wayahudi.  
2. Al-Baqarah, 47.  
3. Al-A’raaf, 140.  
4. Al-Jaathiyah, 16.  
5. Rejea: Tafsir Amthal, juzuu ya 1, uk. 220, Tehran.  
6. Al-Baqarah, 57.  
7. Taz. Tafsir al-Kashif.  
8. Taz. Tafsir Majma‘ al-Bayan, Ibn Kathir, Fakhr Razi n.k.  
9. Al-Maaidah, 60.  
10. Rejea: Mafaatih al-Ghayb (Fakhr Razi), juzuu ya 3, uk. 493.  
11. Aal ‘Imran, 110.  
12. Aal ‘Imran, 33.  
13. Al-An‘aam, 86.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha