Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika muktadha wa kuimarisha nafasi ya hawza na kuchunguza mbinu za kuinua nafasi ya maulamaa katika jamii, mkutano kwa jina la “Hawza Yetu Lucknow na Majukumu Yetu” umefanyika kwa kushirikisha maulamaa, wanafunzi wa fani za dini (ṭullāb), na waumini.
Walioshiriki kikao hiki wamesisitiza ulazima wa kuendelezwa kwa mazungumzo na kushauriana kati ya maulamaa na wasimamizi wa hawza. Mafungamano haya na ushirikiano endelevu umetajwa kuwa hatua yenye athari kubwa katika kutatua matatizo na kuimarisha mshikamano wa kielimu na kidini kwa taasisi za hawza.
Maoni yako