Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kikao chake cha kwanza cha mwaka mpya na viongozi waandamizi wa mihimili mitatu ya dola, alitaja "ufuatiliaji" kuwa kiungo kilichopotea katika njia ya kufanikisha malengo ya nchi.
Vilevile, alisisitiza kuepuka kuwa na matumaini au mashaka ya kupindukia kuhusu matokeo ya mazungumzo ya Oman na akasema: mwenendo wa shughuli za nchi katika kufanikisha malengo katika nyanja zote unapaswa kuendelea kwa kasi zaidi, na hakuna jambo lolote linalopaswa kufungwa kwenye matokeo ya mazungumzo hayo.
Kiongozi wa Mapinduzi alitaja uwekezaji katika uzalishaji kuwa njia bora zaidi ya kukabiliana na vikwazo vya kiuchumi, na akaongeza: kuondoa vikwazo si jambo lililo mikononi mwetu, lakini kuyazima na kuathiri vikwazo hivyo kunatutegemea sisi, na kwa kazi hiyo kuna njia nyingi na uwezo wa ndani unaofaa. Ikiwa lengo hili litafikiwa, basi nchi haitadhurika mbele ya vikwazo.
Alitaja kupanua uhusiano na majirani, vituo vya kiuchumi vya Asia, Afrika na mataifa mengine kuwa jambo muhimu na akasema: jambo hili pia linahitaji ufuatiliaji, hasa kwa ajili ya kubadili baadhi ya mienendo katika ngazi za kati.
Alipokuwa akisisitiza kuepuka "matumaini na mashaka ya kupita kiasi" kuhusu mazungumzo hayo, aliongeza: katika hatua za awali, uamuzi wa nchi wa kushiriki kwenye mazungumzo ulifanyika vizuri. Baada ya hapo pia tunapaswa kuendelea kwa umakini, huku mistari myekundu kwa upande wetu na kwa upande wa pili ikiwa wazi kabisa.
Hadhrat Ayatollah Ali Khamenei aliongeza: mazungumzo yanaweza kufikia matokeo au yasifanikie. Sisi kwa mazungumzo haya hatuna matumaini makubwa wala mashaka makubwa. Bila shaka, tuna mashaka makubwa sana kwa upande wa pili, lakini tuna matumaini makubwa kwa uwezo wetu wenyewe.
Hadhrat Ayatollah Khamenei alihitimisha hotuba yake kwa kunukuu uhalifu wa kihistoria unaofanywa na genge la kihalifu la Kizayuni katika mashambulizi ya makusudi dhidi ya wagonjwa, waandishi wa habari, magari ya wagonjwa, hospitali, watoto na wanawake wenye kudhulumiwa wa Gaza, na akasema: uhalifu huu unahitaji ukatili wa hali ya juu ambao kundi la wahalifu wanaoikalia kwa mabavu ardhi ya Palestina wanamiliki.
Alisema kuwa; harakati ya pamoja ya ulimwengu wa Kiislamu katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na, inapobidi, kijeshi ni hitaji la dharura na akasisitiza: bila shaka, Mwenyezi Mungu atauangushia mjeledi wake juu ya madhalimu hawa, lakini jambo hilo halipunguzi hata kidogo wajibu mzito wa serikali na mataifa.
Maoni yako