Kwa mujibu wa taarifa ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Maher Hammoud, Rais wa Umoja wa Wanazuoni wa Muqawama Duniani, katika hotuba ya sala ya Ijumaa alisema: "Dalili za kurejeshwa kwa uhusiano wa kawaida na ushawishi wa Wazayuni zimefikia kikomo, damu yetu imekuwa ikimwagika katika mito ya Ghaza na kila kona yake, pamoja na sehemu nyingine za Palestina ambazo zimejeruhiwa."
Akaongeza kwa kusema: "Jeshi la jinai la Wazayuni limefikia Idlib, Homs, Hama na Daraa, mahali ambapo mashujaa mashuhuri waliuawa; hadi Saida, ambapo shujaa mmoja kutoka Kikosi cha al-Qassam aliuawa pamoja na mwanawe wa kiume na wa kike katika shambulio la kigaidi, kiasi cha kwamba tulikuwa hatujui kama mashujaa wa aina hii walikuwepo miongoni mwetu, na hapa namkusudia Hassan Farhat na familia yake."
Sheikh Hammoud alieleza: Marekani na Wazayuni wameanza kuingilia siasa za ndani ya Lebanon, kwa mfano, hakuna mgombea hata mmoja aliyejitokeza kuwania nafasi ya uongozi wa Benki kuu ya Lebanon akiwa na mtazamo wa wazi wa kitaifa."
Rais wa Umoja wa Wanazuoni wa Muqawama aliashiria kwamba: "Watu wengi ambao wanataka kujisalimisha na kurejesha uhusiano wa kawaida pamoja na utawala wa Kizayuni hawana uhalali wowote, na kutokuwepo kwa uwiano hakuwezi kutulazimisha kuulaani muqawama."
Mwisho, alisisitiza kwamba: "Kurejesha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni ni mradi ulioshindwa, na khati ya muqawama ndio itakayoibuka na ushindi licha ya mazingira na shinikizo linalo tuzunguka."
Maoni yako