Kwa mujibu wa ripoti ya kundi la tarjama la Shirika la Habari la Hawza, maelfu ya waumini wa Jammu na Kashmir walihudhuria katika matembezi ya Siku ya Quds, huku wakionesha kulihami Taifa lililo dhulumiwa la Palestina.
Matembezi hayo yaliyo ongozwa na Jumuiya ya Kisheria ya mashia wa Jammu na Kashmir, yalionesha umoja, imani, na kujitolea kwao katika suala la Palestina.

Maelfu ya waumini wa Jammu na Kashmir walihudhuria kwa wingi katika matembezi makubwa ya siku ya Quds, huku wakipiga mayowe yaliyo ashiria "Kifo kwa Israeli" na "Uhuru kwa Palestina", kuonyesha mshikamano wao thabiti juu ya Taifa lililo dhulumiwa la Palestina.
Maoni yako