Kwa mujibu wa ripoti kutoka katika kikundi cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Sayyid Sajid Ali Naqvi, Rais wa Shura ya ulama wa kishi’a Pakistan, alitoa tamko lake huku akisisitiza umuhimu wa siku ya Quds na aliwaomba watu wa Pakistan kushiriki kwa wingi Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani kama Siku ya Quds.
Aliashiria uhalifu unaofanywa na wazayuni dhidi ya watu wa Palestina, kwa kusema: "Dhuluma dhidi ya wapalestina imefikia kikomo chake, ukoloni na u-zayuni kwa kushambulia wanawake, watoto, wazee, hospitali, waandishi wa habari na vituo vya msaada wameonyesha sura yao halisi ya kikatili."
Mwanazuoni huyu maarufu wa Pakistan aliweka wazi kuwa: "ukoloni na u-zayuni umeghariki katika uhalifu wao kiasi cha kwamba kwa sasa hawazingatii sheria za kimataifa, mipaka na haki za binadamu."
Akiwaalika watu wa jamii mbalimbali kushiriki kwa wingi katika maandamano, semina, na mikusanyiko ya siku ya Quds, alisisitiza kwa kusema: "Muda wa kuwa Msikiti wa Al-Aqsa haupo huru na watu wa Palestina hawajapata haki zao, maandamano na upinzani utaendelea."
Maoni yako