Jumapili 23 Machi 2025 - 11:37
Kudhihirisha Upendo wa Wapakistani kwa Imam Ali (a.s)

Nchini Pakistan; Kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya kifo cha Imam Ali (a.s), miji ya nchi hiyo iligubikwa na hali ya majonzi. Makundi maalum ya kuomboleza yaliyo andaliwa kwa heshima maalum kutoka sehemu mbali mbali za nchi hii na wapenzi wa Amirul-Mu'minin (a.s), kwa ajili ya kupiga vifua na kusoma maombolezo, yalionesha upendo na heshima yao kwa Amirul-Mu'minina (a.s).

Kwa mujibu wa taarifa ya kikundi cha tarjamah cha Shirika la Habari la Hawza, Kutoka miji midogo hadi miji mikubwa ya Pakistan, marasim ya maombolezo yaliendelea kufanyika huku yakihudhuriwa na watu wengi. Jijini Karachi, kundi maalumu kwa ajili ya maombolezo ya shahada ya Imam Ali (a.s) lilianzia kutoka Nishtar Park.
Waombolezaji walipita katika njia hiyo, huku wakiwa wamejawa huzuni na majonzi, walisoma Nawha zilizo ashiria dhulma alizofanyiwa Imam Ali (a.s) na hatimae swala ya Adhuhuri waliswalia katika mtaa wa Eim Jinnah.
Watu hawa, baada ya kupiti katika njia kuu kuu, walikamilisha maombolezo yao katika Husseiniya ya Wairani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha