Shirika la Habari la Hawza - Mawakibu zimetoka mikoa tofauti, waombolezaji wamejaa huzuni na majonzi kutokana na kumbukumbu ya kifo cha Imamu Ali (a.s). Mawakibu zimeelekea kwenye malalo ya Imamu Ali (a.s) kwa ushiriki wa mazuwaru waliokuja kuomboleza msiba huo. Kawaida mawakibu huomboleza kumbukumbu za vifo vya Ahlulbait (a.s), kikiwemo kifo cha Imamu Ali (a.s).

Mji wa Najafu-Ashrafu umeshuhudia mawakibu za waombolezaji katika malalo ya Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) zikiomboleza kifo chake.
Maoni yako