Shirika la Habari la Hawza - Maafisa wa masuala ya Qur'ani, kidini na kisiasa walihudhuria hafla hiyo katika Ukumbi wa Mosallah Imam Khomeini (RA) Jumatano jioni.
Hafla hiyo ilianza kwa hotuba ya Hujjatul Islam Hamid Reza Arbab Soleimani, Naibu Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu anayeshughulikia masuala ya Qur'ani na Etrat.
Alitoa shukrani kwa wasimamizi na wanaharakati wa Qur'ani kutoka Iran na nchi nyingine kwa mchango wao katika kuandaa maonesho hayo.
Alisema kuwa mwaka huu maonyesho yana sehemu 37, ambapo 28 zinaendeshwa na taasisi mbalimbali.
Akirejelea ushiriki wa nchi 15 katika sehemu ya kimataifa, alisema juhudi zitafanyika kukuza suala la diplomasia ya Qur'ani katika sehemu hiyo.
Mwaka huu, kazi mpya tisa zinazohusiana na Qur'ani na Etrat zitazinduliwa kwenye maonyesho, na pia kutakuwa na majukwaa 58 ya kitaalamu pamoja na vikao vya wataalamu 26.
Katika moja ya siku za mwisho za maonesho, hafla ya 30 ya kuwaheshimu wanaharakati wa Quran itafanyika kwa ushiriki wa rais wa Iran, alibainisha.
Hujjatul Islam Arbab Soleimani pia alisema kuwa katika toleo hili, kipaumbele maalum kinatolewa kwa Etrat (mafundisho ya Maimamu Watoharifu) na Muqawama wa Kiislamu.
"Juhudi zetu katika maonesho, mashindano, na kila tukio la Qur'ani ni kuleta kazi na shughuli zetu karibu zaidi na Qur'ani, kutafakari mafundisho yake, na kuifanya Qur'ani kuwa kiongozi wetu wa mwongozo. Ikiwa juhudi hizi (maonyesho) zinajitokeza katika mwezi wa Ramadhani, ni kwa sababu Ramadhani ni mwezi wa fursa na maendeleo ya binafsi. Kwa hivyo, tunachukua suala la Qur'ani kwa uzito wakati huu."
Waziri wa Utamaduni Seyed Abbas Salehi na pia walihutubia hafla ya ufunguzi.
Katika hotuba yake alisema: "Maonyesho ya Qur'ani yanapaswa kutufahamisha kuhusu miujiza ya Wahyi na kutukurubisha kwenye muujiza wa kimaarifa na wa batini wa Qur'ani."
Akiashiria sifa za Neno la Wahyi, alisema: Qur’ani inatokana na chemchemi ya elimu ya azali, na kwamba wakati vitabu vingine vya mbinguni viliteremshwa mara moja kwa mpigo, Qur'ani Tukufu iliteremsha kwa mpigo na taratibu, na uteremsho wa mpigo ulimhusu Mtume na ule wa taratibu ulikuwa kwa Umma.
Salehi ameongeza kuwa: "Qur'ani ni muujiza utakaodumu hadi Siku ya Kiyama, na pia ni muujiza ambao tunapaswa kuwa karibu nao."
Maonyesho yataendelea hadi Machi 16, 2025. Wale wanaotaka kutembelea tukio hilo la Qur'ani wanaweza kutembelea maonyeso kila siku kuanzia saa 10 jioni hadi saa tano usiku.
Maonyesho ya mwaka huu yanajumuisha programu mbalimbali, zikiwemo vikao maalum, warsha za elimu, mikusanyiko ya Qur'ani, na shughuli maalum kwa watoto na vijana.
Toleo la 32 linaenea kwa takriban mita za mraba 20,000, likihusisha sehemu 37 za maudhui na operesheni.
Maonyesho ya Kimataifa ya Quran ya Tehran huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadan.
Maonyesho hayo yanakusudia kukuza fikra za Qur’ani na kuendeleza shughuli za Qur’ani nchini na duniani kote.
Aidha huonyesha mafanikio ya hivi karibuni ya sekta ya Qur’ani nchini pamoja na aina mbalimbali za bidhaa ambazo ni maalumu kwa ajili ya kukuza Kitabu Kitakatifu.
"Quran; Njia ya Maisha" imechaguliwa kama kaulimbiu ya maonyesho ya mwaka huu.
Chanzo: IQNA
Maoni yako