Jumatatu 3 Machi 2025 - 17:12
Katika zama mpya, Ujumbe wa Seminari za Kiilmu ni mzito zaidi kuliko hapo zamani

Hawza / "Tumeingia katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, na ibada za Mwezi huu zina daraja na viwango tofauti, na wale waliofaulu kuufahamu ukweli na uhakika wa kifalme wa Mwezi huu si sawa (wengine). Bali njia hii haina mwisho, na kila mtu hupitia daraja na viwango tofauti ndani yake".

Kwa mujibu wa ripota wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza Arafi, Mkurugenzi wa Seminari siku ya Jumapili, alipokuwa akitoa pongezi kwa kuwasili kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani alisema: Tunatumai kuwa Mwenyezi Mungu atatusaidia sote kunufaika na baraka za Mwezi huu Mtukufu na kwamba wapendwa wetu wanaofanya bidii katika uwanja wa Harakati za kueneza Ukweli wa Dini watabarikiwa.

Akizungumzia hatua zilizochukuliwa za kutuma Mubalighina zaidi ya 30,000 katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, alisema: Kwa baraka za uongozi, msafara mkubwa na mpana umefanyika kwa uratibu na taasisi mbalimbali.

Akisisitiza umuhimu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Ayatollah Arafi ameongeza kuwa: Tumeingia katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, na ibada za Mwezi huu zina daraja na viwango tofauti, na wale waliofaulu kuufahamu ukweli na uhakika wa kifalme wa Mwezi huu si sawa (wengine). Bali njia hii haina mwisho, na kila mtu hupitia daraja na viwango tofauti ndani yake.

Akirejelea falsafa ya ibada, Ayatollah Arafi alifafanua: Ibada inapaswa kuhusisha nafsi nzima ya mtu na kumtoa nje ya dhahiri. Kwa hakika, ibada kamili ina maana ya umiliki wa Mwanadamu juu yake mwenyewe na utimilifu wa ibada ya moyo, ambayo ina maana ya kutakasa moyo kutokana na kushikamana na Ulimwengu wa kiwiliwili (Ulimwengu wa Kimaada).

Aidha ametaja fadhila maalumu za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kusema: Ramadhani ni fursa ya kipekee ya kunufaika na neema za Mwenyezi Mungu. Mwezi huu una majina na sifa zaidi ya mia moja katika Aya na riwaya mbalimbali, na ufahamu sahihi wa Mwezi huu humsaidia mtu kuwa katika njia ya ibada.

Mkurugenzi wa Seminari (Hawzah) za Kiilmu aliongeza zaidi: Seminari ni mwongozo wa kuelewa katika ibada na matibabu ya kiroho ya Wanadamu. Ni lazima kwanza tujiboresha sisi wenyewe kisha tuwasaidie wengine. Miongoni mwa ibada muhimu sana katika Mwezi huu ni funga ya moyo, ambayo ni ya juu zaidi kuliko funga ya kimwili. Katika suala hili, mtu anapaswa kusafisha moyo wake kutoka kwenye uhusiano wote wa kidunia na kumzingatia Mwenyezi Mungu tu. Saumu ya aina hii ni ya juu zaidi kuliko funga ya dhahiri na inahitaji uangalifu na hesabu ya uangalifu wa mawazo na nia ya mtu.

Kisha Ayatollah Arafi akaashiria ulazima wa kutilia maanani matatizo ya Ulimwengu mpya na kusema:

Ulimwengu wa leo umeweka majukumu makubwa katika Seminari zenye maendeleo ya haraka ya kyisayansi na kiteknolojia.

Sayansi mpya kama vile Fizikia ya Quantum na Akili ya Bandia zimefanya mabadiliko makubwa katika maisha ya Mwanadamu.

Katika zama mpya, ujumbe wa Hawza (Seminari) ni mzito zaidi kuliko hapo awali.

Ameongeza kuwa: Leo hii, kasi ya maendeleo ya Kisayansi ni kwamba mtu anaweza kupata ujuzi katika muda mfupi ambao haukuweza kupatikana kwa karne nyingi. Kasi hii ya mabadiliko inahitaji uangalizi maalum kwa mafundisho ya Kiislamu na uimarishaji wa mitazamo ya kidini dhidi ya maendeleo haya.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha