Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Muhammad Al-Fahdawi, mmoja wa viongozi wa Muungano wa Azm nchini Iraq, alisema siku ya Jumanne kuwa; vitisho vya mashambulizi ya ardhini ya pamoja kati ya utawala wa Kizayuni na Marekani dhidi ya Iran si chochote zaidi ya «kimbunga cha muda mfupi» kinacholenga kuiwekea Tehran shinikizo ili kuilazimisha kukubali makubaliano mapya katika suala la nyuklia kwa manufaa ya serikali ya Trump.
Alionya kuwa endapo kutafanyika mashambulizi ya ardhini kwa lengo la kuukalia kimabavu Mlango-Bahari wa Hormuz na Kisiwa cha Khark, majeshi ya utawala wa Kizayuni na Marekani yatakumbana na kushindwa kusiko na mfano na kwa kiwango kikubwa.
Katika maelezo yake, Al-Fahdawi alisema: «Matamshi ya Trump na timu yake kuhusu maandalizi ya kufanya mashambulizi ya ardhini dhidi ya Iran kwa uratibu na Israel yatakuwa na matokeo mabaya sana, na Iran itapata ushindi kwa namna ambayo haitarajiwi.
«Habari zinazosambazwa kuhusu kuchukuliwa maamuzi ya haraka ya kufanya mashambulizi ya ardhini dhidi ya Iran hazina msingi wowote. Marekani haitathubutu kuingia katika jaribio hilo la kijeshi kutokana na gharama kubwa za vita hivyo.»
Majeshi ya utawala wa Kizayuni na Marekani yatakumbana na anguko kubwa
Al-Fahdawi aliongeza kuwa; iwapo majeshi ya utawala wa Kizayuni na Marekani yataamua kufanya operesheni ya ardhini kwa lengo la kuukalia kimabavu Mlango-Bahari wa Hormuz na Kisiwa cha Khark, yatakumbana na kushindwa kukubwa na kusiko na mfano, huku Iran ikiwa mshindi.
Alifafanua kuwa; Iran bado ina uwezo mkubwa wa kijeshi katika mapambano ya ardhini, ambao unaweza kuyashinda majeshi vamizi. Aidha, katika kulinda ardhi yake, mizani ya nguvu itakuwa upande wa Iran, kwani majeshi yake hayatasalimu amri hadi yatakapofikia ushindi.
Maoni yako