Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Abdul Ahmad al-Dulaimi, mwanachama wa muungano wa Siyada, katika matamshi yake amesisitiza kuwa; Washington imeipa Israel idhini ya kutumia anga ya Iraq ili kuishambulia Iran.
Al-Dulaimi amesema: «Kufunguliwa anga ya Iraq kwa ajili ya safari za ndege za Israel kumefanyika kwa idhini ya Marekani, ili kuwezesha uchokozi dhidi ya Iran. Hii ni sehemu ya mpango unaoongozwa na Washington kwa lengo la kuisukuma Iraq na kuilazimisha kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo, kwani Marekani imeshindwa katika jitihada zake za kuizuia serikali ya Iraq isiutambue adui wa Kizayuni».
Ameongeza kuwa: «Lengo la uchokozi wa Wazayuni dhidi ya Iran ni kuharibu miundombinu yake ya nyuklia, hatua hiyo inalenga kuuwezesha utawala wa Kizayuni kulitishia eneo la Mashariki ya Kati kwa kuhodhi silaha za nyuklia».
Aidha, amebainisha kuwa kuhamishia uwanja wa mapambano katika ardhi ya Iraq ni mpango wa Kizayuni unaolenga kuiangamiza nchi hiyo na kuilazimisha kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo.
Al-Dulaimi amehitimisha kwa kusisitiza kuwa: «Ukiukaji wa anga ya Iraq unaofanywa na ndege za Israel na kuishambulia Iran ni tukio linaloweka mfano hatari katika ukiukaji wa mamlaka na uhuru wa Iraq. Kwa hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje inapaswa kuchukua hatua madhubuti katika suala hili».
Maoni yako