Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Misri yenye mwelekeo wa Kiarabu imekuwa daima na historia adhimu katika kuunga mkono Muqawama na wapambanaji wa Muqawama; huku ikitegemea historia yake ya kimapinduzi, kimapambano na ya utaifa katika kutetea haki za Waarabu na, katika kiini chake, haki ya Palestina; mahali ambapo dhamiri ya wananchi na fikra yake ya kimapambano iliungana na Harakati ya Kiislamu ya Muqawama nchini Lebanon, chini ya uongozi wa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Shahidi Mtakatifu, Sayyid Hassan Nasrullah (qds).
Katika muktadha huo, Kamal Abu Aita, mwanaharakati wa wafanyakazi na mwanasiasa wa Misri, na Waziri wa zamani wa Kazi, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa pili tangia kupata Shahada Sayyid Hassan Nasrullah (qds), alituma ujumbe kwenye tovuti ya habari ya «Al-Ahed», ambapo alikumbushia misimamo na nafasi yake katika mapambano kati ya Waarabu na Uzayuni.
Abu Aita alisema: “Katika historia ya mwanadamu, kuna watu ambao hawarudiwi, Mwenyezi Mungu amrehemu Sayyid Hassan Nasrullah, alikuwa mwakilishi wa matakwa ya sisi sote; mimi ni Mnassiri [mfuasi wa Gamal Abdel Nasser], na kwa sasa ninamuona kuwa mwakilishi wa matakwa yangu mwenyewe na mwakilishi wa matakwa ya mkondo wa utaifa wa Kiarabu katika suala la mapambano ya Kiarabu na Uzayuni.”
Aliongeza: “Mwenyezi Mungu amrehemu na aupe Umma wetu viongozi watakaosimamia mchakato wa mapambano dhidi ya adui wa kwanza wa Umma huu kwa ufanisi uleule, kwa werevu uleule na kwa msimamo uleule, Mwenyezi Mungu amrehemu na atujaalie sote badala njema.”
Maoni yako