Ijumaa 18 Septemba 2026 - 17:30
Kushindwa Utegemezi wa Nguvu za Kigeni wa Saudia, ni Anguko la Kimkakati; Kurekebisha Mahusiano na Israel Itakuwa Kujitoa Kafara

Hawzah/ Samir Ayoub amesisitiza kwamba njia sahihi ya Saudi Arabia na nchi za eneo hilo kujinasua kutoka kwenye mtego wa Yemen ni kuanzisha mawasiliano na mazungumzo na kushughulikia sababu za mzozo, ambazo kuu zaidi ni kuondoa mzingiro dhidi ya wananchi wa Yemen, kurejesha mambo katika hali ya kawaida na kutoingilia masuala ya ndani ya Yemen.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Samir Ayoub, mwandishi na mwandishi wa habari wa Lebanon anayeishi Moscow, katika mahojiano na kituo cha “Al-Masirah”, alisisitiza: “Kilichotokea katika Bahari Nyekundu kilisababisha kushindwa mkakati na sera ya Kiarabu ambayo ingeweza kutekelezwa kwa ushirikiano na Marekani kwa lengo la kulishambulia Jeshi la Yemen.”

Ayoub alibainisha: “Vikosi vya Wanajeshi wa Yemen, ambavyo vimeshiriki katika kuunga mkono wananchi wa Palestina na kuunga mkono Muqawama nchini Lebanon, na ambavyo vimekuwa chanzo kikuu cha kuilenga nguzo ya kiuchumi ya utawala wa Kizayuni katika Bahari Nyekundu, vilikabiliwa na shambulio lililolenga kupunguza uwezo wao; lakini kilichotokea kilikuwa kinyume kabisa.”

Alirejelea: “Vikosi vya Wanajeshi wa Yemen vilifanya operesheni ya mapema ambayo ilifunga njia kwa yeyote aliyekuwa na nia ya kulidhuru karata hii yenye nguvu iliyopo katika eneo hili, ambayo ina uwezo wa kuendelea kuwaunga mkono wananchi wa Palestina na wananchi wa Lebanon katika Muqawama wao dhidi ya uvamizi wa Kizayuni.”

Ayoub alieleza: “Kipindi cha kuunga mkono Ukanda wa Ghaza na wananchi wa Palestina kilisisitiza kwamba; upande wa Yemen una uwezo wa kufanya mashambulizi makali na yenye kuamua, ambayo hayakomei katika juhudi za kijeshi za Israel pekee, bali pia yanalenga nguzo yake kuu, ambayo ni uchumi.”

Alisema: “Wasiwasi wa sasa wa Wazayuni unahusiana na uwezekano wa kudhoofishwa kwa upande wa kusini wa utawala huo kutoka upande wa Bahari Nyekundu; kwa sababu vikosi vya Yemen vinatishia meli na vifaa vinavyofika kwa utawala wa Israel, pamoja na meli na maslahi ya nchi zinazoweka mzingiro dhidi ya wananchi wa Yemen, hasa Saudi Arabia.”

Aliongeza: “Kuendelea kwa tishio hili kunaweka maslahi ya kiuchumi ya utawala huo na nchi zinazoshiriki katika mzingiro dhidi ya Yemen katika changamoto za moja kwa moja katika eneo la Bahari Nyekundu.”

Mchambuzi huyo wa Lebanon alisisitiza: “Saudi Arabia na nchi za Ghuba ya Uajemi, ikiwa zinataka maslahi ya nchi zao na kurejea kwa usalama na utulivu, zinapaswa badala ya kukimbilia nje ya nchi na kuomba msaada kwa nguvu za kigeni ili zijitetee, kukabiliana na migogoro ya eneo hilo kupitia mazungumzo na kushughulikia masuala yaliyopo, pamoja na kuheshimu maslahi na haki za wananchi wao.”

Alitaja kosa hilo la kwanza na la kuangamiza kuwa ni uwepo wa kambi za kijeshi za Marekani katika nchi hizo, na kueleza: “Kambi hizi hazikujengwa kwa ajili ya kuzisaidia nchi hizo, bali zilijengwa kwa ajili ya kuitumikia Israel, na wakati wa vita vilivyoendeshwa dhidi ya Iran, pamoja na wakati wa vita dhidi ya wananchi wa Yemen, zilichukua nafasi ya mstari wa ulinzi kwa ajili yake.”

Kuhusu kutokuwa na athari halisi kwa makubaliano ya Saudi Arabia na Uturuki pamoja na Pakistan, Ayoub alieleza: “Msingi wa makubaliano haya ni kuzilinda nchi hizo iwapo zitakabiliwa na shambulio au uvamizi. Hata hivyo, kinachotokea leo si uvamizi dhidi ya Saudi Arabia, bali ni ulinzi wa Yemen kwa ajili ya mamlaka yake, maslahi yake na kuvunja mzingiro dhidi ya wananchi wa Yemen.”

Aliendelea: “Wananchi wa Yemen si washambuliaji, bali wanajilinda wenyewe. Kwa sababu hiyo, Pakistan na Uturuki walilizingatia jambo hili na wakaamua kutokuingilia kijeshi. Taarifa zinazosambazwa na utawala wa Israel kuhusu makubaliano haya ni jaribio la kuutuliza upande wa Saudi Arabia, hasa baada ya Marekani kukataa kutoa msaada au kutekeleza mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen, na pia baada ya msimamo wa Uingereza uliotangaza kwamba inaendelea kuchunguza hali hiyo.”

Alibainisha: “Nchi nyingine hazitaki kuingia katika vita ambavyo si vyao, wala kurejea tena katika mtego ambao hapo awali waliingia na kushindwa kufikia malengo waliyokuwa wameyataka.”

Katika muktadha huo, Ayoub alirejelea kwamba: “Utawala wa Kizayuni unajaribu kuijengea Saudi Arabia na nchi za eneo hilo dhana kwamba yeye ndiye chombo pekee kinachoweza kuwalinda na kulinda maslahi yao. Kushughulikia kwa uzito kauli hizi kunaweza kugeuka kuwa kosa la kihistoria na kimkakati.”

Alisisitiza: “Nchi za eneo hili hazipaswi kudanganywa na madai ya utawala huo kwamba una uwezo wa kuzilinda, kwa sababu hata kujilinda wenyewe hauwezi; nchi za Ulaya na mfumo wa ulinzi wa Marekani zilijitokeza kumsaidia na kukabiliana na makombora yaliyokuwa yakiwafikia kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na pia kutoka Yemen.”

Alieleza: “Kauli za Israel kuhusu kuyalinda mataifa ya eneo si chochote zaidi ya jaribio la kutumia suala hilo kisiasa na kuingiza dhana ya uwezekano wa kushirikiana nayo kwa ajili ya kuhifadhi usalama na maslahi yao, ilhali lengo halisi ni kuyashinikiza yaendelee na njia ya mikataba ya kurekebisha mahusiano, ambayo Marekani na utawala wa Kizayuni wanaitaka.”

Kurekebisha Mahusiano na Israel Itakuwa ni Kujitoa Kafara Saudi Arabia, na Kuongeza Mvutano Kutazidhuru Nchi za Eneo

Ayoub aliona uwezekano wa Saudi Arabia kufanikiwa katika kuelekea kwenye ushirikiano wa moja kwa moja na utawala wa Kizayuni kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen na maslahi ya Yemen kuwa ni mdogo, na akasisitiza: “Chaguo kama hilo kwa Saudi Arabia litakuwa sawa na kujitoa kafara.”

Alisema: “Utawala wa Kizayuni unajaribu kutumia mkwamo wa Saudi Arabia kupitia makamanda wake wa kijeshi na vyombo vyake vya kijasusi, kwa uratibu na Marekani pamoja na baadhi ya nchi za eneo, lakini hauwezi kutoa msaada wa kweli kwa Saudi Arabia.”

Kwa msisitizo mkubwa alisema: “Ustahimilivu, nguvu na kasi ya harakati za wananchi wa Yemen hatimaye zitasababisha kuondolewa kwa mzingiro dhidi ya wananchi hao na kurejea kwenye mazungumzo pamoja na makubaliano yatakayoheshimu maslahi ya nchi za eneo na haki za wananchi wa Yemen.”

Ayoub alisisitiza: “Njia sahihi ya Saudi Arabia na nchi za eneo kujinasua kutoka katika mzozo wa Yemen ni kuanzisha mawasiliano na mazungumzo na kushughulikia sababu za mzozo, ambazo kuu zaidi ni kuondoa mzingiro dhidi ya wananchi wa Yemen, kurejesha mambo katika hali ya kawaida na kutoingilia masuala ya ndani ya Yemen. Wananchi wa Yemen wana uelewa mkubwa zaidi kuhusu masuala ya nchi yao na matatizo wanayokabiliana nayo, na wana uwezo wa kuyatatua bila uingiliaji wa kigeni.”

Kwa mara nyingine alisisitiza: “Kutegemea utawala wa Kizayuni hakutaleta matokeo yoyote, hasa kwa kuwa utawala huo ni dhaifu mara kadhaa zaidi ya Marekani; nchi ambayo ina meli za kivita zilizoko katika eneo hili, lakini ilikataa kutoa msaada kwa sababu haitaki, baada ya uzoefu wa awali na kushindwa kufikia malengo yake, kuingia tena katika mtego wa Yemen.”

Ayoub katika muktadha huo alisisitiza: “Hatua za kijeshi haziwezi kuzisaidia nchi za eneo, bali zitasababisha kuangamizwa kwao.” Alitoa wito wa kurejea kwenye mazungumzo na kutafuta suluhisho kwa mambo yote yaliyosababisha mzozo huo. Alitahadharisha: “Kuongeza mvutano kunaweza kusababisha kufungwa kwa Mlango wa Bab al-Mandab na huenda hata njia ya baharini kuelekea Mfereji wa Suez ikalengwa; jambo ambalo uchumi wa dunia hauwezi kulivumilia.”

Alieleza: “Mashambulizi ambayo Saudi Arabia iliyskabili yalikuwa makali na mazito na yalikuwa na athari kubwa kwa nchi hiyo, hasa katika eneo la uchumi, suala hili halihusu Saudi Arabia pekee tena, bali uchumi wa dunia nao unaathiriwa nalo.”

Ayoub alitoa wito wa kuiwekea shinikizo Saudi Arabia na nchi zinazoweka mzingiro dhidi ya wananchi wa Yemen, ili badala ya kuelekea katika kuongeza mvutano au kuomba msaada kutoka kwa nchi ambazo hazitafuti kuzitumikia nchi hizo, bali zinataka kuhakikisha maslahi yao wenyewe na maslahi ya utawala wa Israel, zichukue hatua za kutatua matatizo na kushughulikia sababu pamoja na mizizi ya mzozo.

Alimalizia kauli zake kwa kusisitiza kwamba mtazamo wa nchi nyingi zenye ushawishi unaelekea katika kutatua mzozo kupitia mazungumzo, badala ya uingiliaji wa kijeshi; jambo ambalo linazipa nchi za eneo hilo fursa ya kurejea katika hali ya utulivu, hata ikiwa utulivu huo utakuwa wa muda, na kutumikia maslahi ya pande zote.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha