Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Arak, Ayatullah Muhsin Araki jana, akiwa miongoni mwa wananchi wa Arak katika hafla ya kumbukizi ya siku ya 40 ya msafara wa mazishi ya mwili mtakatifu wa Bwana Shahidi wa Iran, iliyofanyika katika Muswalla ya Beit al-Muqaddas, huku akielezea umuhimu wa falsafa ya kuandaliwa hafla ya Arubaini, amesema: “Kuandaliwa hafla ya Arubaini ya Hadhrat Sayyid al-Shuhadaa (as), au Arubaini ya mazishi ya mwili mtakatifu wa Imam wetu Shahidi, kwa hakika kuna maana ya kufanya upya ahadi na njia ya haki na ukweli, pamoja na kutekeleza agano la kiapo cha Mwenyezi Mungu.”
Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza aliongeza kusema: “Hii ndio maana ya kutajwa, katika matini za kidini, Ziara ya Arubaini kuwa miongoni mwa alama za muumini.”
Alisema kwamba; kuandaliwa hafla hii kuna maana ya kutekeleza agano la kudumu na uaminifu kwa Imam Shahidi, na akaongeza: “Kila mmoja ajue kwamba maana ya kulipiza damu ya kiongozi wa mashahidi si tu kutibu maumivu ya mioyo yetu; bali kwa hakika kisasi hiki ni kwa manufaa ya ubinadamu na haki, na kwa ajili ya kutimizwa kwa muqawama dhidi ya madhalimu wa historia, ili kuzuia udhalili na fedheha ya upande wa haki.”
Ayatullah Araki aliendelea kusema: “Miongoni mwa hatari zinazotishia Mapinduzi haya ni kwamba, wakati adui anaposhindwa kufuta jina la Maimamu wawili wa Mapinduzi, hujaribu kupotosha malengo makuu ya Mapinduzi.”
Pia alibainisha kwamba: “Muqawama hauna maana ya kusimama dhidi ya maadui binafsi; bali una maana ya kusimama dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, tunapozungumzia kulipiza kisasi, kwa hakika tunatangaza kwamba jamii ya wanadamu inapaswa kuondokana na sababu za dhuluma na ukandamizaji pamoja na uvimbe wa saratani, ili ubinadamu uonje maana ya uhuru wa kweli.”
Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi aliongeza kuwa: “Kwa hiyo, kama vile uadui wa Maasumina (as) dhidi ya watu kama Muawiya na Yazid haukuwa ugomvi binafsi, sisi pia hatuna ugomvi wa kibinafsi na maadui wetu; bali tunawachukia kwa sababu wao ni maadui wa jamii nzima ya wanadamu.”
Ayatullah Araki, alipokuwa akirejea aya tukufu: «و لا تهنوا و تدعو الی السلم و انتم الاعلو» alisema: “Kwa masikitiko, siku hizi baadhi ya watu, kutokana na kutofahamu misingi ya Uislamu, wanazungumzia amani na adui, wakati ambapo amani na maadui wa wanadamu haina maana.”
Aliongeza kuwa: “Kwa hiyo, vita na jihadi dhidi ya wale ambao, kama wanyama wakali, wanatishia ubinadamu, si jambo la kulaumiwa tu; bali ni jambo takatifu.”
Ayatullah Araki alisema: “Vita vya leo dhidi ya maadui ni kuondoa vijidudu vinavyoiua jamii ya wanadamu, na kazi ya wapiganaji katika kupambana na maadui ni kama kazi ya madaktari katika kuzuia magonjwa au kupambana na magonjwa.”
Mwalimu wa Hawza ya Qom, mwishoni, alisisitiza kuwa: “Leo tunawaahidi Maasumina wote (as), na vilevile mashahidi pamoja na kiongozi wetu shahidi, kwamba; tutalipiza kisasi cha damu zao.”
Maoni yako