Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kidini wa Kiislamu ulitangaza katika taarifa yake kwamba; unapinga kwa nguvu hatua ambazo utawala wa Kizayuni na ngome ya uvamizi wa Kizayuni unajaribu kuzisukuma mbele kwa lengo la kubadilisha mpangilio wa kisiasa wa eneo hilo chini ya shinikizo la nje.
Walisema kwamba; ikiwa hatua hizi zitaendelea huku Israel ikiendelea na mauaji ya halaiki na uvamizi wake huko Ghaza na maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, hatua hiyo itamaanisha kuipa uhalali wa kisiasa jinai ya utawala wa Kizayuni unaomwaga damu.
Muungano wa Wanazuoni wa Kiislamu uliwataka viongozi wa taasisi za kidini katika ulimwengu mzima wa Kiislamu kuchukua msimamo ulio wazi kuhusu suala hili na kukusanyika kwa uratibu mkubwa zaidi kati ya nchi zenye Waislamu wengi kwa ajili ya kuunga mkono haki za Wapalestina.
Taasisi hiyo ilisema kwamba; aina yoyote ya uthabiti wa kudumu katika suala la Palestina inahitaji kushughulikia misingi ya tatizo hilo, likiwemo suala la ukaliaji wa mabavu na kuwafanya watu kuwa wakimbizi.
Chanzo: Safa News.
Maoni yako