Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, tuzo ya papa ya “Ordine Piano” ni tuzo ya heshima ya Kiti Kitakatifu ambayo ilianzishwa mwaka 1847 Miladia na Papa Pius wa Tisa. Tuzo hii inahesabiwa kuwa miongoni mwa tuzo za juu kabisa za kishujaa za Vatican, na kwa kawaida hutolewa kwa mabalozi na watu mashuhuri ambao wamekuwa na mchango katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia pamoja na kuhudumia amani na mazungumzo.
Tuzo hii imetolewa kwa balozi wa Iran katika hali ambayo misimamo ya hivi karibuni ya Papa Leo wa Kumi na Nne ya kutetea haki kwa kulaani mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, haiwezi kutenganishwa na juhudi za ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Vatican katika kufafanua ujumbe wa amani, uadilifu na kupinga uchochezi wa vita.


Maoni yako